Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waarabu wamkomalia Mayele

MABINGWA wa Kombe la Shirikisho la Afrika, RS Barkane ya Morocco imemkomalia straika wa Yanga, Fiston Mayele ikitaka kumsajili baada ya kuona dili lao na Victorien Adebayor wa Asec Mimosas ya Ivory Coast kupata ugumu flani.
Kocha Mkuu wa Berkane, Florent Ibenge ndiye anayedaiwa kuchochea usajili wa Mayale anayeongoza orodha ya mabao katika Ligi Kuu Bara sambamba na George Mpole wa Geita Gold ili kama ikitokea dili la Adebayor aliyekuwa akihitajika na Simba likikwama asitoke patupu.
Chanzo cha habari kutoka Morrocco kimeripoti taarifa hii,  ikisemkena kuwa ndani ya wiki hii Barkane inaweza kuanza mazungumzo rasmi na Yanga ili kumbeba Mayele, ingawa klabu hiyo nayo inampigia hesabu kumuongezea mkataba mpya juu ya alionao sasa wa mwaka mmoja.
Juni 4, mwaka juu Mwanaspoti ililiripoti kuwa Mayele ameuambia uongozi ili aweze kuendelea kubaki Jangwani ni lazima aongezewe mkataba na marupurupu kwenye mshahara wake wa sasa. Mayele kwa sasa ana mkataba uliosaliwa na mwaka mmoja.
“Ofa ni kweli ipo na sisi bado tunamhitaji kutokana na mafanikio aliyotupa ndani ya mwaka mmoja alioitumikia Yanga baada ya kumwambia hivyo ameutaka uongozi umuongeze mshahara na mkataba wa mwaka mmoja ili abaki kuwa na miwili tena,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;
“Mchakato wa makubaliano mapya bado haujaanza tunasubiri mwisho wa msimu kabla ya mchjezaji hajaondoka kwenda mapumziko, kujiandaa na msimu mpya.
Chanzo hicho kilisema kuna uwezekano mkubwa wa kukubaliana na ofa za Mayele kutokana na umuhimu wake kwenye timu, ukizingatia mbele kuna michuano ya CAF.
“Ndani ya misimu minne mfululizo tumevunja timu kwa kusajijli sajili wachezaji hilo hatutaki lijirudie msimu huu tutafanya kila mbinu kuhakikisha wachezaji muhimu wanabaki na tutaongeza wengine ili kukiboresha zaidi kikosi,” kilisema chanzo hicho.