Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waoga mamilioni M-Bet, yaitakia kheri Simba

Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi (Katikati) akipozi na washindi, Abdallah Segatwa (kulia) na Mesharam Bakunda baada ya kukabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh175.3 baada ya kushinda droo ya Perfect 12.

Dar es Salaam. Kampuni ya mchezo ya kubashiri ya M-Bet Tanzania imewazawadia washindi wawili kila mmoja Sh175.3 millioni baada ya kubashiri kwa usahihi matokeo ya ligi mbalimbali duniani kupitia mchezo wa Perfect 12.

Washindi hao ni Mesharam Bakunda na Abdallah Segatwa ambao walizawadiwa fedha zao jana Alhamisi, Februari 23, 2023 katika halfa fupi iliyofanyika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi alisema kuwa wanajisikia fahari kubwa kubadili maisha ya mashabiki hao wa soka ambao wote ni wafuasi wa klabu ya Arsenal.

Mushi alisema kuwa washindi hao wawili wanaungana na wengine wengi katika nyumba ya mabingwa na kuwaomba mashabiki wa soka kujaribu bahati zao kwa kubashiri na kampuni yao.

“Mbali ya kubadili maisha ya washindi wetu kupitia kubashiri michezo, pia tunajisikia fahari kuchangia asilimia 20 ya kodi ya ushindi ambayo inaigia moja kwa moja serikalini. Sisi ni walipa kodi wazuri wa Serikali na tunachangia maendeleo,” alisema Mushi ambaye pia ameitakia Simba mafanikio mema katika mchezo wake dhidi ya Vipers ya Uganda utakaochezwa kesho.

Kwa upande wake, Bakunda ambaye pia ni shabiki wa Yanga alisema kuwa hakuamini kushinda kiasi hicho cha fedha kwa kutumia Sh1, 000 tu.  Alisema kuwa amekuwa akibashiri mara kwa mara kwani ameshuhudia washindi kadhaa wakishinda fedha nyingi kupitia kampuni hiyo.

Naye Segatwa alisema kuwa hakukata tamaa katika safari yake ya kubashiri na mara kadhaa alikuwa anabashiri na kushinda fedha kidogo.

“Mimi mkulima, nitatumia fedha hizi kwa ajili ya kuendelza kilimo, kuboresha nyumba na kusomesha watoto wangu. Nimekuwa nikibashiriki na kupata hela ndogo ndogo. Nilipopigiwa simu na kuambiwa kuwa nimeshinda zaidi ya milioni 100, sikuamini na nilidhani ni ndoto,” alisema Segatwa.