Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wawili ‘waipasua kichwa’ Yanga

KICHWA Pict


KUELEKEA mwishoni mwa msimu wa 2025/26, Yanga imeendelea kufanya maandalizi ya kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao kwa kusaka wachezaji watakaoongeza ushindani ndani ya kikosi hicho. Safari hii, mabosi wa klabu hiyo wameelekeza macho yao kwa viungo wawili wa Singida Black Stars.


Licha ya dirisha la usajili kutokuwa limefunguliwa rasmi na msimu wa ligi bado haujamalizika, klabu mbalimbali tayari zimeanza kufanya mazungumzo ya usajili kwa siri, huku baadhi ya wachezaji wakisaini mikataba ya awali.


Taarifa zinaeleza kuwa Yanga imeanza mchakato wa kuangalia viungo wazawa wanaoweza kuongeza nguvu katika eneo la kiungo. Kwa sasa, majina mawili yapo mezani huku viongozi wa klabu hiyo wakifanya tathmini ya nani anayefaa zaidi kusajiliwa.

Wachezaji wanaotajwa kuwa katika rada za Yanga ni Ahmed Pipino na Khalid Habib maarufu kama’Gego’, wote kutoka Singida Black Stars.

Pipino alianza msimu wa 2025/26 akiwa KMC kabla ya kujiunga na Singida Black Stars kwa mkataba wa miaka mitatu. Kabla ya kusaini mkataba huo, alihusishwa na Simba na Azam FC, lakini akaamua kujiunga na Singida ambapo ni kati ya wazawa wachache wanaopata nafasi kikosini.

Chanzo cha ndani kiliieleza Mwanaspoti kuwa Yanga bado haijafanya uamuzi wa mwisho kuhusu mchezaji itakayemsajili kati ya wawili hao, kwani wote wameonyesha kiwango kizuri na bado wana umri mdogo.

“Yanga ikikamilisha tathmini yake itawasilisha ombi rasmi kwa Singida Black Stars kwa ajili ya kumsajili mmoja kati ya hao. Klabu ina mpango wa kuongeza idadi ya viungo wazawa kutokana na ukweli kwamba viungo wa kigeni waliopo wanaendelea kufanya vizuri,”  kilisema chanzo hicho.


Kazi inawasubiri

Kiungo yeyote atakayesajiliwa atalazimika kupambana kupata nafasi katika kikosi cha kwanza kutokana na ushindani uliopo. Kwa sasa, Duke Abuya kutoka Kenya na Mohamed Damaro na Mudathir Yahaya, wanaendelea kung’ara katika eneo hilo na wamekuwa chaguo muhimu kwa benchi la ufundi.