Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga yashinda ikiweka rekodi rekodi tatu

Muktasari:

  • Rekodi ya kwanza inamuhusu mfungaji wa mabao mawili, Clement Mzize ambaye sasa amefikisha mabao 13 akiwa kinara wa ufungaji Ligi Kuu Bara kwa sasa.

MABINGWA watetezi, Yanga wameendelea kunyatia ubingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Fountain Gate, katika mchezo uliopigwa Jumatatu hii kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliopo Babati mkoani Manyara huku ushindi huo uliofanya Yanga kufikisha pointi 70, umeweka rekodi tatu ndani ya kikosi hicho.

Rekodi ya kwanza inamuhusu mfungaji wa mabao mawili, Clement Mzize ambaye sasa amefikisha mabao 13 akiwa kinara wa ufungaji Ligi Kuu Bara kwa sasa.

Kwa kufikisha idadi hiyo ya mabao, maana yake Mzize amefunga mara mbili zaidi ya ilivyokuwa msimu uliopita ambapo alimaliza na mabao sita na asisti saba.

Rekodi ya pili ni ya Yanga kucheza mechi 16 mfululizo za msimu huu bila ya kupoteza, tangu mara ya mwisho kikosi hicho kilipochapwa mabao 3-1 dhidi ya Tabora United, Novemba 7, 2024.

Katika michezo hiyo 16, Yanga imeshinda 15 huku mmoja pekee ukiisha kwa suluhu (0-0) ambao ulikuwa ni dhidi ya maafande wa JKT Tanzania. Rekodi hiyo ya kucheza michezo 16 ya Ligi Kuu bila ya kupoteza, imeifikia pia ya Simba ambayo nayo imecheza idadi sawa ya mechi kama hizo, ambapo kikosi hicho tangu kichapwe na Yanga bao 1-0, Oktoba 19, 2024, hakijapoteza tena hadi leo.

Katika michezo hiyo 16 ya Simba ambayo imecheza mfululizo ya Ligi Kuu Bara bila ya kupoteza, imeshinda 14, huku miwili pekee dhidi ya Fountain Gate na Azam FC ikiisha sare.

Rekodi ya tatu ya msimu ni ile ya Yanga kufikisha michezo 14 ya ugenini kati ya 26 iliyocheza katika Ligi Kuu Bara bila ya kupoteza ikishinda 13 na sare moja.

Ushindi umeifanya Yanga kuifunga Fountain Gate jumla ya mabao 9-0 msimu huu, baada ya mechi ya kwanza kuichapa 5-0 Desemba 29, 2024.

Clement Mzize alianza kuitanguliza Yanga dakika ya 38, baada ya kipa wa Fountain Gate raia wa Nigeria, John Noble kutema mpira. Noble kwa mara ya pili alifanya makosa baada ya kushindwa kuumiliki mpira na kupiga pasi fupi iliyonaswa na Stephane Aziz KI aliyepiga bao la pili na lake la nane msimu huu katika dakika ya 43. 

Mzize akafunga bao la tatu dakika ya 70, akipokea pasi ya mtokeabenchini Jonathan Ikangalombo na kufikisha mabao 13. msimu huu akiwapiku Prince Dube na Jean Charles Ahoua wa Simba (12).  Clatous Chama aliyeingia kuchukua nafasi ya Aziz Ki, alihitimisha ushindi kwa bao la frii-kiki.