Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Staa wa Yanga kuwania uenyekiti AFC Leopards SC

AMBANI Pict
AMBANI Pict

Bonface Ambani, gwiji wa soka nchini Kenya na mchezaji wa zamani wa AFC Leopards, amezindua rasmi ilani yake ya kampeni iitwayo “IPOSIKU” leo Juni 26, 2025, katika ukumbi wa KCB Simba jijini Nairobi.

Ambani anawania nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu ya AFC Leopards, ambapo uchaguzi utafanyika Jumapili, Juni 29. Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi wa klabu, wanasiasa, na wadau mbalimbali waliomuunga mkono kwa dhati.

Ilani ya IPOSIKU, yenye kaulimbiu “Kurudisha Uhai Kwenye Mchezo”, inalenga kujenga upya imani, uadilifu na umaarufu wa klabu hiyo. Ambani alieleza kuwa lengo kuu ni kuhuisha utawala bora, kushirikisha mashabiki, na kurejesha heshima ya AFC Leopards ambayo imedorora kwa zaidi ya miongo miwili kutokana na uongozi dhaifu.

Ilani hiyo inatambua maeneo manne ya kipaumbele: kufanya mabadiliko ya nembo na muundo wa klabu, kuimarisha miundombinu, kuendeleza uhusiano na matawi/mashabiki, pamoja na kuhakikisha usimamizi wa fedha kwa uwazi na ufanisi.

Ambani na timu yake ya #IPOSIKU wameandaa mpango wa hatua 11 ujulikanao kama “Starting XI” ambao unajikita katika uwajibikaji na ushirikishwaji wa wadau wote.

Baadhi ya mambo muhimu katika Starting XI ni pamoja na utawala bora, maendeleo ya soka la wanawake na vijana, utafutaji wa vyanzo mbalimbali vya mapato, uboreshaji wa ustawi wa wachezaji, pamoja na kuanzishwa kwa mifumo rasmi ya mafunzo kwa makocha, waamuzi na watendaji. Pia ilani inasisitiza marekebisho ya katiba ya klabu ili kuhakikisha uwiano sahihi wa madaraka na uwazi wa maamuzi.

Viongozi wa soka na waliowahi kufanya kazi na Ambani waliunga mkono azma yake ya kuwaongoza AFC Leopards, wakimtaja kama kiongozi mwenye maono, weledi na mapenzi ya kweli kwa klabu.

Ambani aliwataka wanachama wote wa AFC Leopards kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya Jumapili na kuchagua uongozi utakaorejesha heshima ya klabu hiyo kongwe ya Kenya.