Bosnich apata ahueni

SYDNEY, AUSTRALIA: Kipa wa zamani wa Manchester United, Mark Bosnich ambaye aliwahishwa hospitali Jumanne wiki hii baada ya kuugua ghafla, kwa sasa mchezaji huyo anaendelea vizuri.
Bosnich (52), aliweka picha kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii akiwa kitandani huku akitabasamu kuonyesha kwamba anaendelea vizuri.

Kisha baada ya picha hiyo mkongwe huyo aliandika kwamba angetolewa hospitali jana na kupumzika hadi Ijumaa kabla ya kurejea kwenye majukumu yake ya uchambuzi wa mechi mbalimbali anaoufanya nchini Australia.
Baada ya kuweka picha na maelezo hayo watu wengi waliandika ujumbe wa kumuombea apone haraka.
Akiwa na Man United alifanikiwa kuchukua taji la Ligi Kuu England 2000 kisha 2001 aliondoka kikosini.