Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Al-Ittihad yaanza kujisogeza karibu kwa Mohamed Salah

Muktasari:

  • Salah ambaye hadi sasa ndiye anaongoza kwa utupiaji msimu huu, anapewa nafasi kubwa ya kuondoka kwa sababu Liverpool haijaonyesha nia ya kutaka kumsainisha mkataba mpya wakati muda ukizidi kuyoyoma. Matajiri wa Saudi walitaka kumsajili tangu dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana lakini ikashindikana licha ya kuweka mezani zaidi ya Pauni 150 milioni kama ada ya uhamisho na mshahara unaokaribia Pauni 70 milioni.

MATAJIRI wa Al-Ittihad ya Saudi Arabia wana imani kubwa kuwa mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah, mwenye umri wa miaka 32, atajiunga nao katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi mara baada ya mkataba wake na Liverpool kumalizika.

Salah ambaye hadi sasa ndiye anaongoza kwa utupiaji msimu huu, anapewa nafasi kubwa ya kuondoka kwa sababu Liverpool haijaonyesha nia ya kutaka kumsainisha mkataba mpya wakati muda ukizidi kuyoyoma. Matajiri wa Saudi walitaka kumsajili tangu dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana lakini ikashindikana licha ya kuweka mezani zaidi ya Pauni 150 milioni kama ada ya uhamisho na mshahara unaokaribia Pauni 70 milioni.


Liam Delap

MANCHESTER United imeongeza juhudi katika kumsajili mshambuliaji wa Ipswich Town, Liam Delap mwenye umri wa miaka 22, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Liam ambaye mkataba wake unamalizika 2029 ili kuipata huduma yake Ipswich inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 40 milioni kama ada ya uhamisho. Katika msimu huu amefunga mabao 10 katika mechi 31 za michuano yote.


James Trafford

NEWCASTLE United bado ina nia ya kumsajili kipa wa Burnley, James Trafford, 22, katika dirisha lijalo la kiangazi ili kuboresha na kuongeza ushindani katika lango. Trafford ni miongoni mwa mastaa tegemeo katika kikosi cha Burnley na msimu huu amecheza mechi 38 za michuano yote na kuruhusu mabao 11. Mkataba wa mchezaji huyo unatarajiwa kumalizika ifikapo 2027.


Joao Pedro

BRIGHTON inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 100 milioni kutoka timu yoyote itakayohitaji saini ya mshambuliaji raia wa Brazil, Joao Pedro katika dirisha lijalo. Mbali ya Pedro, Brighton pia ipo tayari kumuuza kiungo wake wa kimataifa wa Cameroon, Carlos Baleba ikiwa itapata ofa nzuri. Mastaa hao wote wanawindwa na Liverpool, Newcastle United na Chelsea.


Bernardo Silva

KIUNGO wa Manchester City na timu ya taifa ya  wa Ureno, Bernardo Silva, 30, anadaiwa kuwa katika mpango wa kuondoka dirisha lijalo na kutafuta changamoto mpya sehemu nyingine baada kudumu kwa muda mrefu katika kikosi hicho. Taarifa zinaeleza kuna uwezekano mkubwa akatimkia Saudi Arabia ambako timu nyingi zinahitaji huduma yake kwa ofa nono.


Hugo Ekitike

CRYSTAL Palace pia inaangalia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt, Hugo Ekitike, 22, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ikiwa straika kutoka Ufaransa, Jean Mateta anayehusishwa na timu mbalimbali kubwa Ulaya kutokana na kiwango chake alichoonyesha tangu kuanza kwa msimu huu. Ekitike pia anawindwa na vigogo kibao ikiwemo Man United.


Evan Ndicka

ARSENAL, Newcastle United na Nottingham Forest ni miongoni mwa timu zilizoonyesha nia ya kutaka kumsajili beki kisiki wa Roma na Ivory Coast, Evan Ndicka dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Ripoti kutoka Italia imefichua kuwa, Roma ipo tayari kumuuza supastaa huyo lakini ikiwa timu inayomtaka italipa kiasi kisichopungua Euro 40 milioni.


Thierno Barry

CHELSEA inafikiria kutoa Euro 40 milioni kwenda Villarreal kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa timu hiyo mwenye umri wa miaka 22, Thierno Barry, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Thierno ambaye msimu huu amecheza mechi 33 za michuano yote na kufunga mabao 17, mkataba wake unatarajiwa kumalizika 2029.