Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ancelotti akabidhiwa mikoba Brazil

ANCELOTTi Pict

Muktasari:

  • Mtaliano huyo mwenye umri wa miaka 65, amekubali kwenda kuinoa miamba hiyo mabingwa mara tano wa dunia na ataanza majukumu yake Mei 26 baada ya kukamilika kwa msimu wa La Liga.

RIO DE JANEIRO, BRAZIL: HATIMAYE, Carlo Ancelotti amethibitishwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya soka ya Brazil.

Mtaliano huyo mwenye umri wa miaka 65, amekubali kwenda kuinoa miamba hiyo mabingwa mara tano wa dunia na ataanza majukumu yake Mei 26 baada ya kukamilika kwa msimu wa La Liga.

Kocha huyo aliyewahi kuzinoa pia Chelsea na Everton na klabu nyingine nyingi za Ulaya amekuwa chaguo la kwanza la Brazil tangu ilipomfuta kazi Dorival Jr, Machi mwaka huu.

Dorival alipoteza ajira yake baada ya kichapo cha mabao 4-1 kwenye mechi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026 mbele ya mahasimu wao Argentina.

Kutokana na dili hilo, Ancelotti atakuwa kocha wa kwanza wa kigeni kuinoa timu ya taifa ya Brazil, Selecao. Ancelotti ataanza kazi yake mwezi ujao kwenye mechi za kufuzu dhidi ya Ecuador na Paraguay.

Na mkataba wake utafika tamati mwishoni mwa fainali za Kombe la Dunia 2026 kama ilivyo kwa mkataba wa Mjerumani, Thomas Tuchel kwenye timu ya taifa ya England.

Brazil kwa sasa inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa timu 10 kutoka ukanda wa Amerika Kusini na timu sita za juu ndizo zinazofuzu fainali za Kombe la Dunia.

Lakini, iko mbele kwa tofauti ya pointi tano dhidi ya timu inayoshika nafasi ya saba, Venezuela.

Mabosi wa FA ya Brazil walizungumza na mabosi wa Real Madrid akiwamo rais wa klabu hiyo, Florentino Perez kumruhusu Ancelotti kabla ya mwishoni mwa msimu wa klabu hiyo.

Na klabu hiyo ya Bernabeu sasa imepanga kumtambulisha Xabi Alonso kama mrithi wa Ancelotti katika kikosi cha Real Madrid kitakachokwenda kwenye fainali za Kombe la Dunia la Klabu huko Marekani.

Ancelotti aliipa Real Madrid mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na La Liga mara mbili. Alishinda pia Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili alipokuwa na AC Milan na alishinda jumla ya mataji ya ligi za ndani mara sita, alipotamba na timu za Chelsea, PSG na Bayern Munich.