Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arsenal kuibamiza Madrid mbona kawaida

UEFA Pict

Muktasari:

  • Katika michuano hiyo hadi sasa timu hizi zimekutana mara tatu ambapo Arsenal imeshinda mbili na mchezo mmoja ukamalizika kwa matokeo ya 0-0.

LONDON, ENGLAND: JANA Arsenal ilifanikiwa kuichapa Real Madrid mabao 3-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kilikuwa kipigo cha kushtusha kwa mashabiki wa soka kutokana na ubora wa wachezaji wa Madrid.

Hata hivyo, historia inaonyesha, Arsenal kupata ushindi mbele ya Madrid hususani katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya sio jambo la kushangaza kwani imeshazoea kufanya hivyo.

Katika michuano hiyo hadi sasa timu hizi zimekutana mara tatu ambapo Arsenal imeshinda mbili na mchezo mmoja ukamalizika kwa matokeo ya 0-0.

Mbali ya ukweli kwamba Madrid haijawahi kupata ushindi wowote kwenye michuano ya Ulaya dhidi ya Arsenal, pia haijawahi kuitoa timu hiyo zilipokutana katika hatua ya mtoano wala kufunga bao.

Mara ya kwanza kukutana kwenye hatua ya mtoano ilikuwa ni msimu wa 2005-2006 ambapo mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora uliopigwa Dimba la Santiago Bernabeu ulimalizika kwa Arsenal kushinda bao 1-0 kisha marudiano ukaisha kwa 0-0.

Mwaka huu tena wamekutana katika mtoano ingawa ni hatua ya robo fainali na hadi sasa Arsenal inaonekana kwamba itaendeleza ubabe wake kutokana na idadi kubwa ya mabao ambayo imeyapata katika mechi ya mkondo wa kwanza.

Katika mabao matatu ya Arsenal, mawili yalifungwa na Declan Rice dakika ya 58 na 70 kupitia mpira wa faulo, kisha Mikel Merino akafunga bao la tatu dakika ya 75.

Madrid ilipata pigo katika dakika za mwisho baada ya kiungo wake Eduardo Camavinga kuonyeshwa kadi ya pili ya njani iliyoambatana na nyekundu dakika nne ya nyongeza.

Wakati Madrid ikichapika ugenini, Bayern Munch ikiwa nyumbani Allianz Arena ambapo patatumika kwa ajili ya mchezo wa fainali, ilipokea kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Inter Milan.

Hatua hiyo ya robo fainali itaendelea leo ambapo Barcelona itaumana na Borussia Dortmund kuanzia saa 4:00 usiku wakati PSG ikiwa nyumbani itaikaribisha Aston Villa muda huo huo.