Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta afunguka hali ya Saka

Muktasari:

  • Saka alitolewa nje ya uwanja baada ya kushindwa kuendelea kucheza katika mechi ya Ligi Kuu England kutokana na faulo aliyofanyiwa na beki wa Ipswich, Leif Davis, ambaye alipewa kadi nyekundu ya moja kwa moja.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta amewahakikishia mashabiki wa Arsenal kuwa staa wa timu hiyo, Bukayo Saka hakuumia vibaya licha ya faulo mbali aliyofanyiwa na kulazimu atolewe katika mchezo wa wikiendi iliyopita dhidi ya Ipswich Town.

Saka alitolewa nje ya uwanja baada ya kushindwa kuendelea kucheza katika mechi ya Ligi Kuu England kutokana na faulo aliyofanyiwa na beki wa Ipswich, Leif Davis, ambaye alipewa kadi nyekundu ya moja kwa moja.

Nyota huyo wa England alionekana akiwa na barafu kwenye kifundo cha mguu kwenye benchi na baadaye alionekana akichechemea alipokuwa akipanda basi la timu. Mashabiki walikuwa na hofu kutokana na umuhimu wake na baadhi walienda mbali wakidai huenda ametoneshwa jeraha ambalo limetoka kumuweka nje kwa muda mrefu.

“(Beki huyo)alimkata kutoka nyuma. Sidhani kama ilikuwa amekusudia kucheza vile, lakini bila shaka ni mchezo wa hatari kwa sababu huwezi hata kujikinga na kumuona mpinzani akiwa anakuja... mwamuzi alifanya uamuzi sahihi.. (Saka) alikuwa na maumivu kidogo, lakini si maj makubwa.. yuko sawa,” alisema Arteta.

Saka alicheza mechi yake ya kwanza mwaka huu,  Aprili Mosi alipoingia kama mchezaji wa akiba katika ushindi wa Arsenal dhidi ya Fulham baada ya kuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu akiuguza majeraha aliyofanyiwa upasuaji wa msuli wa paja.

Wiki moja baadaye, aliwasumbua Real Madrid katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa, kabla ya kufunga bao muhimu kwenye ushindi wa kihistoria Uwanja wa Bernabeu katika mchezo wa marudiano.

Hofu ya benchi la ufundi na mashabiki ilikuwa kumkosa mechi ijayo dhidi ya PSG.