Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta aisukia mkakati maalum PSG

ARTETA Pict

Muktasari:

  • Arsenal itakuwa na michezo kadhaa ya kucheza kwenye  Ligi Kuu kabla ya kuikaribisha PSG kwenyeUwanja wa Emirates.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta ameanza kazi  ya kupanga namna atakavyoingia kwenye mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya PSG wiki ujao, ikiwamo kumtumia Leandro Trossard kama mshambuliaji wa kati.

Arsenal itakuwa na michezo kadhaa ya kucheza kwenye  Ligi Kuu kabla ya kuikaribisha PSG kwenyeUwanja wa Emirates.

Trossard aliongoza safu ya ushambuliaji dhidi ya Ipswich  na uamuzi huo ulizaa matunda baada ya Mbelgiji huyo kufunga mabao mawili. Arteta amefunguka anaweza akamchezesha tena staa huyo kwenye eneo hilo kwa sababu ameonyesha utayari na uwezo wa kucheza vizuri.

Arsenal inapambana kuziba mapengo katika safu yao ya ushambuliaji kutokana na majeraha yanayowasumbua mastaa waliozoeleka kucheza eneo hilo.

“Ndiyo, bila shaka yuko tayari kucheza katika nafasi yoyote. Tunahitaji kufanya marekebisho fulani, sio kwa sababu ya PSG, bali kutokana na hali tuliyonayo, tunamkosa  Thomas Partey na wachezaji wengine. Lakini jambo zuri ni timu inaonyesha kuzoea na wachezaji fulani wanaweza kucheza nafasi tofauti. Hilo ni muhimu sana, hasa tukizingatia idadi ya wachezaji tulionao kwa sasa ni ndogo,” alisema Arteta alipoulizwa ikiwa atamchezesha Trossard kama mshambuliaji wa kati dhidi ya PSG.

Arteta pia anaweza kubadilisha nafasi ya Mikel Merino dhidi ya PSG baada ya  Mhispania huyo kucheza mbele zaidi dhidi ya Ipswich kutokana na kukosekana kwa Thomas Partey.

Alipoulizwa kuhusu jinsi atakavyoingia  katika mchezo huo, Arteta alijibu:

“Lazima tuwatumie wachezaji 11, na tufanye mabadiliko manne au matano. Tutaona hali za wachezaji zitakuwaje katika siku chache zijazo. Kitu kizuri ni wanapenda kucheza, wanapenda kasi ya michezo kama hiyo mikubwa. Pia tumeshazoea kucheza kila baada ya siku tatu, wachezaji wanahitaji kuendelea  na kwa bahati nzuri hatuna mechi wikendi hii, hivyo tutakuwa na muda wa kupumua, acha tuone hali itakuwaje Jumatano.”