Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Arteta atikiswa tena, majeraha yakikiandama kikosi

Muktasari:

  • Mabeki hao wawili washindwa kumaliza mechi hiyo, ambayo Arsenal ilishinda 2-1 na kuendeleza vita yao katika kufukuzia ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu na hivyo kumtikisa kocha Arteta kutokana na pigo hilo.

LISBON, ENGLAND: KOCHA mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta, amesema wanasubiri kwa hamu taarifa za kuhusu mastaa wake mawili Gabriel na Jurrien Timber waliopata majeraha katika mechi ya ushindi dhidi ya Fulham iliyopigwa Emirates, Jumanne usiku.

Mabeki hao wawili washindwa kumaliza mechi hiyo, ambayo Arsenal ilishinda 2-1 na kuendeleza vita yao katika kufukuzia ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu na hivyo kumtikisa kocha Arteta kutokana na pigo hilo.

Zikiwa zimechezwa dakika zisizozidi 15, beki wa kati Gabriel alionekana kushika sehemu ya nyuma ya mguu wake akionyesha kwamba hayo ni majeraha ya misuli. Na sekunde chache baadaye, alinyanyua mkono wake juu kuonyesha kwamba ameumia kabla ya kukaa chini uwanjani akionekana kuwa na maumivu makali na hivyo kufanyiwa mabadiliko.

Timber alipatiwa matibabu kwenye kipindi cha kwanza na alikaa kitako tena kwenye kipindi cha pili na hivyo kumlazimisha kocha Arteta kufanya mabadiliko mengine kwenye kikosi chake cha Arsenal.

Jakub Kiwior na Leandro Trossard waliingia kuchukua nafasi za mabeki hao, huku kocha Arteta akisubiri kufahamu ukubwa wa tatizo la maumivu yanayowakabili mastaa wake hao.

“Hatujui ni kitu gani kitaendelea. Tutawafanyia uchunguzi zaidi,” alisema Arteta.

“Gabi alihisi maumivu kwenye misuli yake. Hatufahamu tatizo ni kubwa kiasi gani. Jurrien naye alionekana kuwa na shida mapema. Alishindwa kuendelea.”

Akizungumzia majeraha ya Gabriel, wakati anatangaza talkSPORT, straika wa zamani wa West Ham United, Dean Ashton alisema: “Ni pigo kubwa. Yeye na (William) Saliba ni mabeki bora kwenye Ligi Kuu England. Ni tishio sana kwenye mipira ya adhabu pia. Nilichukua alivyocheza dhidi ya Adama Traore, ule ulikuwa mtihani mzito kwa Gabriel.”

Mchezaji mwenzake Gabrield, kiungo Declan Rice anaamini majeraha hayo hayawezi kuwa makubwa sana kama inavyodhaniwa, aliposema: “Sijui kilichotokea, natumaini atakuwa vizuri kwa sababu yeye ni mmoja wa wachezaji bora kabisa msimu huu na tunamhitaji kwenye mechi kubwa na nyakati kubwa.”

Wakati Arsenal ikifukuzia ubingwa ubingwa wa Ligi Kuu England, ambao unaonekana kuwa na kipengele kwao, majeruhi hao wanaiweka kwenye wakati mgumu katika mechi yao ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid wiki ijayo. Arsenal itaikaribisha Los Blancos Jumanne ijayo uwanjani Emirates.


Arsenal kisha itakwenda kurudiana na Real huko Bernabeu siku nane baadaye katika kipute cha robo fainali. Kwenye Ligi Kuu England, mchezo wao ujao watakipiga na Everton.

Gabriel na Timber sasa wataungana na Kai Havertz na Gabriel Jesus kwenye orodha ya mastaa majeruhi watakaokosekana uwanjani kwa muda mrefu, sambamba na Takehiro Tomiyasu na Riccardo Calafiori.

Katika mchezo huo wa Fulham, Arsenal ilifurahia kurudi uwanjani kwa supastaa wao, Bukayo Saka, ambaye alifunga bao lake la kwanza baada ya siku 101, katika ushindi wa 2-1, ambapo bao la kwanza la miamba hiyo inayonolewa na Arteta, lilifungwa na kiungo wa Kihispaniola, Mikel Merino. Bao la kujifariji la Fulham lilifungwa na Rodrigo Muniz.