Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barca bingwa LaLiga, Espanyol haijapenda

BARCA Pict

Muktasari:

  • Barca ilihitaji ushindi kwenye mechi hiyo ili kuwakata maini wapinzani wao Real Madrid waliokuwa wakifukuzia ubingwa pia, lakini sasa chama hiko la kocha Hansi Flick limeweka pengo la pointi saba kileleni na mechi bado mbili msimu kumalizika.

BARCELONA, HISPANIA: BARCELONA imebeba ubingwa wa La Liga msimu huu baada ya kuichapa Espanyol na kufikisha pointi ambazo hakuna timu nyingine itazifikia kwenye mchakamchaka huo.

Barca ilihitaji ushindi kwenye mechi hiyo ili kuwakata maini wapinzani wao Real Madrid waliokuwa wakifukuzia ubingwa pia, lakini sasa chama hiko la kocha Hansi Flick limeweka pengo la pointi saba kileleni na mechi bado mbili msimu kumalizika.

Bao maridadi kutoka kwa Lamine Yamal kwenye kipindi cha pili, kabla ya kupika jingine yaliifanya Barcelona kushinda 2-0 ugenini na kufikisha pointi ambazo Los Blancos haiwezi kuzifikia na hivyo itaachana na kocha wake Carlo Ancelotti bila ya taji lolote msimu huu.

Lakini, mechi hiyo ya ubingwa kwa Barcelona ilikuwa na tukio baya nje ya uwanja baada ya gari moja kugonga mashabiki wa Espanyol na kujeruhi 13. Tukio hilo la nje ya uwanja lilisababisha mechi isimame kwa muda. Na baada ya matokeo kwa 0-0 hadi mapumziko, kinda wa maajabu wa Barcelona, Yamal alifanya mambo yake kipindi cha pili na kufunga kwa staili tamu dakika ya 53.

Kisha Fermin Lopez alikuja kufunga bao la pili baada ya pasi ya Yamal kuihakikishia taji hilo la La Liga Barcelona na kuanza kusherehea kwenye uwanja wa mahasimu wao hao, kitu ambacho kiliwakera wenyeji na kuamua kufungulia mabomba ya maji ya kumwagilia uwanja.

Espanyol ilifungulia mabomba hayo kuamua kuwaogesha wachezaji wa Barcelona ili watoke uwanja, wasiendelee na sherehe zao za ubingwa. Ushindi huo kwa Barca ulikuba baada ya miaka miwili na siku moja tangu ilipofanya kama hivyo wakati ilipobeba ubingwa uwanjani RCDE mwaka 2023.

Mwaka 2023, wakati wachezaji wa Barca walipokuwa wakishangilia ubingwa kwenye uwanja wa mahasimu wao, walivamiwa na wahuni wa Espanyol wakijaribu kuwazuia.

Kocha wa sasa wa Barca, Hansi Flick hakutaka tukio kama hilo litokee tena wakati huu, hivyo alikuwa akiwapa ishara wachezaji wake waingie vyumbani baada ya filimbi ya mwisho. Lakini, wachezaji walionekana kutoelewa na kushangilia uwanjani. Jambo hilo liliwakera wachezaji wa Espanyol, kabla ya kufunguliwa mabomba ya maji ili wachezaji watoke uwanjani, lakini bado wachezaji Alejandro Balde, Pau Victor, Andreas Christensen na Dani Olmo waliendelea kushangilia kwenye maji.