Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barcelona waanza kumnyatia Julian Alvarez

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Alvarez ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2030, msimu huu amecheza mechi 50 za michuano yote, amefunga mabao 27 na kutoa asisti tano.

BARCELONA wanapanga kufanya usajili wa mshambuliaji wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Argentina, Julian Alvarez, 25, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ikiwa ni katika harakati zao za kujiandaa na maisha bila ya straika wao raia wa Poland, Robert Lewandowski, mwenye miaka 36.

Alvarez ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2030, msimu huu amecheza mechi 50 za michuano yote, amefunga mabao 27 na kutoa asisti tano.

Mabosi wa Barca wanaona kuwa staa wao Lewandowski umri unakwenda kumtupa mkono na wanataka kutafuta mbadala wake kabla staa huyo hajaondoka.

Hata hivyo, haionekani ikiwa Atletico iko tayari kumwachia fundi huyu ambaye ni miongoni mwa wachezaji wao tegemeo.

Kocha Diego Simeone anaonekana kumkubali sana Muargentina mwenzake huyo ambaye ameshinda takriban mataji yote likiwamo Kombe la Dunia, Copa America, Ligi ya Mabingwa Ulaya, EPL nk.


Adam Wharton

LIVERPOOL wanajaribu kumshawishi kiungo wa Crystal Palace, Adam Wharton, 21, ili akubali kujiunga nao katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Ripoti zinaeleza, Wharton mwenye umri wa miaka 21, anaweza kuuzwa lakini kwa kiasi kisichopungua Pauni 50 milioni.

Livepool imedhamiria kuimarisha kikosi baada ya kufanikisha kuwapa mikataba mipya nyota wake Mohamed Salah na Virgil van Dijk.


Andre Onana

NEOM ya Saudi Arabia imeanza mazungumzo na wawakilishi wa Manchester United na kipa wa Cameroon, Andre Onana, mwenye umri wa miaka 29.

Ripoti za hivi karibuni zimefichua kwamba Onana ni mmoja kati ya mastaa wanaoweza kuuzwa mwisho wa msimu huu ambapo kumekuwa na ofa kadhaa kutoka Saudia lakini fundi huyo wa kimataifa wa Cameroon bado anataka kuendelea kucheza soka la kiushindani.


Tomas Soucek

KOCHA wa Everton, David Moyes, amewasilisha jina la kiungo wa West Ham na timu ya taifa ya Jamhuri ya Czech, Tomas Soucek, 30, akitaka asajiliwe katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Soucek ambaye ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha West Ham, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.


Lucas Paqueta

MABOSI wa West Ham wako tayari kumuuza kiungo wao wa kimataifa wa Brazil, Lucas Paqueta, mwenye umri wa miaka 27, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ikiwa ni sehemu ya kukusanya pesa kwa ajili kwa ajili ya kuboresha kikosi chao.

Paqueta ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027, msimu huu amecheza mechi 33 za michuano yote na kufunga mabao matano.


Leroy Sane

WINGA wa Bayern Munich, Leroy Sane, mwenye miaka 29, yuko mbioni kusaini mkataba mpya na timu hiyo ya Bundesliga ikiwa ni baada ya mazungumzo ya wiki kadhaa kati ya wawakilishi wake na mabosi wa timu hiyo. Sane ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu, awali alikuwa akihusishwa kuondoka na Arsenal na Liverpool ndio zilipewa nafasi kubwa ya kumpata.


Callum Hudson-Odoi

ROMA, Napoli na timu mbili za Ligi Kuu England ziko katika mazungumzo na wawakilishi wa Nottingham Forest, kwa ajili ya kuipata saini ya winga wa timu hiyo mwenye umri wa miaka 24, Callum Hudson-Odoi, ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao. Msimu huu amecheza mechi 32, amefunga mabao matano na kutoa asisti tatu.


Tammy Abraham

AC Milan wanafanya mazungumzo na AS Roma kuhusu uwezekano wa kumsainisha mkataba wa kudumu straika wa timu hiyo raia wa England, Tammy Abraham, ambaye anacheza kwa mkopo katika kikosi chao.

Tammy ambaye akiwa na Milan msimu huu amefunga mabao 10 katika mechi 43 za michuano yote, mkataba wake wa sasa na Roma unatarajiwa kumalizika 2027.