Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bernardo Silva aingia anga za Barcelona

Muktasari:

  • Ripoti zinadai Man City haina mpango wa kumuuza fundi huyu lakini ikiwa Barca itawasilisha ofa ya kumsajili na yeye mwenyewe akakubali, hawatomzuia kuondoka.

KIUNGO wa Manchester City na timu ya taifa ya Ureno, Bernardo Silva, 30, ni miongoni mwa mastaa ambao mabosi wa Barcelona wamepanga kuwasajili katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Ripoti zinadai Man City haina mpango wa kumuuza fundi huyu lakini ikiwa Barca itawasilisha ofa ya kumsajili na yeye mwenyewe akakubali, hawatomzuia kuondoka.

Hata hivyo, ili kuipata huduma yake, Barca itatakiwa kumshawishi fundi huyu akubali kuchukua mshahara mdogo tofauti na ule anaoupata kwa sasa akiwa na Man City.

Mkataba wa sasa wa Bernardo anatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu ujao, tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 42 za michuano yote, amefunga mabao matatu na kutoa asisti nne.


Lorenzo Lucca

MANCHESTER United imefikia hatua nzuri katika mazungumzo na mshambuliaji kutoka Udinese, Lorenzo Lucca, 24, ambaye imepanga kumsajili dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Fundi huyu wa kimataifa wa Italia, amelivutia benchi la ufundi la Man United kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu kuanza kwa msimu huu na hadi sasa amefunga mabao 10 katika mechi 30 alizocheza na ni mmoja wa wachezaji tegrmeo wa kikosi hicho.


Dejan Kulusevski

TOTTENHAM imeanza mazungumzo na wakala wa kiungo wao raia wa Sweden, Dejan Kulusevski, 24, ili kumsainisha mkataba mpya na kumzuia asiondoke katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi na vigogo kibao wameonyesha nia ya kumsajili ikiwamo AC Milan na Napoli. Kocha wa Spurs, Ange Postecoglu bado ana mipango na Dejan na hataki kuona akiondoka. Mkataba wake unamalizika mwaka 2028 amekuwa muhimu kikosini hapo.


Pedri

MANCHESTER City imeanza mazungumzo na wawakilishi wa  kiungo wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Pedri ambaye ni mmoja ya mastaa ambao kocha Pep Guardiola anaona wanaweza kusaidia eneo lao la kiungo ikiwa watamsajili. Licha ya nia yao hiyo, ripoti zinaeleza Barca haina mpango wa kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22.


Hugo Larsson

ARSENAL inataka kuipiku Manchester City katika vita ya kuiwania saini ya kiungo wa Entrach Frankfurt na timu ya taifa ya Sweden,  Hugo Larsson, 20, ambaye timu yake inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 50 milioni ili kumuuza. Timu nyingi zimekuwa zikihusishwa na fundi huyu tangu dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana lakini zilishindwa kwa wakati huo kutokana na bei yake.


Rodrygo

CHELSEA imeendelea kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Real Madrid kwa ajili ya kumsajili winga wao na timu hiyo na Brazil, Rodrygo, mwenye umri wa miaka 24, dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Rodrygo ni miongoni mwa wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Madrid, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.


Nicolo Barella

LIVERPOOL inajiandaa kutuma ofa kwenda Inter Milan kumsajili kiungo wa timu hiyo na Italia, Nicolo Barella, 28, dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Barella ni mmoja wa mastaa tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Inter na msimu huu amecheza mechi 42 za michuano yote na kufunga mabao matatu, mkataba wake unamalizika mwaka 2029.


Liam Delap

EVERTON imeungana na timu nyinginw za Ligi Kuu England kuisaka saini ya straika wa Ipswich Town na tiju ya taifa ya England kwa vijana wenye umri chini ya miaka 21, Liam Delap, 22, dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Delap ni mmoja kati wa mastraika walioonyesha kiwango bora msimu huu na amefunga mabao 12 katika mechi 34.