Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Carragher: Alexander-Arnold hapaswi kuanza Liverpool

Muktasari:

  • Beki huyo wa kulia, ambaye mkataba wake na Liverpool unamalizika mwishoni mwa msimu huu, amehusishwa kuwa karibu kujiunga na Real Madrid, wakati mastaa wenzale ambao mikataba yao ilikuwa ikimalizika mwisho wa msimu huu Mohamed Salah na Virgil van Dijk wameshasaini tayari. 

LIVERPOOL, ENGLAND: LEJENDI wa Liverpool, Jamie Carragher amesisitiza beki wa timu hiyo Trent Alexander-Arnold hapaswi kuanza tena katika kikosi cha Liverpool ikiwa hajatoa majibu kama anataka kuondoka au kubaki.

Beki huyo wa kulia, ambaye mkataba wake na Liverpool unamalizika mwishoni mwa msimu huu, amehusishwa kuwa karibu kujiunga na Real Madrid, wakati mastaa wenzale ambao mikataba yao ilikuwa ikimalizika mwisho wa msimu huu Mohamed Salah na Virgil van Dijk wameshasaini tayari. 

Trent alirejea kikosini kutoka kwenye jeraha Jumapili, na akafunga bao pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Leicester City iliyoshuka daraja rasmi baada ya kichapo hicho. Licha ya kufunga bao hilo na kuonekana mwenye furaha kubwa, Carragher alisema kwamba beki huyo hapaswi kuanza tena ikiwa hajatoa kauli juu ya kukubali kubaki katika kikosi hicho kwa muda mrefu.

“Kama Trent hajamwambia kocha kuwa atabakia msimu ujao, basi hatakiwi kuanza mechi yoyote,” alisema Carragher.

Mchambuzi mwenzake na mchezaji wa zamani wa Manchester City, Micah Richards alimjibu Carragher kwa kumuuliza Alexander-Arnold asianzishwe hata kwenye mechi moja kwa ajili ya kumuaga kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa? Carragher akajibu: “Liverpool sio timu inayotoa heshima ya kumuaga mchezaji.”

Nyota huyo wa zamani wa Liverpool alisena kocha Arne Slot anapaswa kumpa kipaumbele beki chipukizi Conor Bradley, akisisitiza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 anahitaji uzoefu kabla ya kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza msimu ujao iwapo Trent ataondoka kwenda Real Madrid.

Liverpool wanaonekana kuwa tayari wameshajihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu England 2024-25 wakihitaji ushindi mechi moja  katika mechi tano zilizosalia. Carragher alisisitiza kuwa mechi zilizobaki zinapaswa kutumika kumpima Bradley ili kuamua kama klabu inapaswa kusaka beki mpya wa kulia badala ya kumpa Alexander-Arnold heshima ya kuagwa kwa hisia.

Baada ya mchezo wa Jumapili iliyopita dhidi ya Leicester, Trent aliulizwa kuhusu hatma yake akasema: ““Sitazungumzia kuhusu hatma yangu kwa sasa, lakini nafurahia hizi siku nilizonazo... kufunga mabao, kushinda mechi na kushinda mataji. Ninafurahi kuwa sehemu ya mafanikio haya.”