Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Euro 10 milioni kumng’oa Alonso Leverkusen

ALONSO Pict

Muktasari:

  • Alonso ameonyesha uwezo mkubwa kama kocha, licha ya kuwa bado hana uzoefu wa kutosha, msimu uliopita aliiwezesha Leverkusen kuchukua taji la Bundesliga wakiwa wamepoteza mechi moja tu, pia wakafika fainali ya  Europa League.

MADRID, HISPANIA: REAL Madrid italazimika kulipa Euro 10 milioni ili kuvunja mkataba wa Kocha wa Bayer Leverkusen, Xabi Alonso inayohusishwa naye kwa muda mrefu,

Alonso ameonyesha uwezo mkubwa kama kocha, licha ya kuwa bado hana uzoefu wa kutosha, msimu uliopita aliiwezesha Leverkusen kuchukua taji la Bundesliga wakiwa wamepoteza mechi moja tu, pia wakafika fainali ya  Europa League.

Ufanisi huo ulimfanya thamani yake ipande haraka na  timu nyingi kubwa Ulaya zikiwemo  Liverpool na Real Madrid zilihitaji kumsajili mwaka jana lakini alikataa na kuendelea kuitumikia Leverkusen.

Kwa sasa Alonso, 43, ambaye amewahi kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Madrid mwaka 2014, anapewa nafasi kubwa ya kuziba pengo linalotarajiwa kuachwa wazi na Carlo Ancelotti anayeweza kuondoka mwisho wa msimu huu.

Kwa mujibu wa gazeti la Bild, licha ya kuwa Alonso anaelewana sana na Mkurugenzi Mtendaji wa Leverkusen, Fernando Carro, ikiwa Madrid itamhitaji italazimkka kutoa kiasi hicho cha fedha kama fidia.

Ancelotti anatarajiwa kuondoka Madrid baada ya fainali ya Copa del Rey itakayopigwa Aprili 26. Mabingwa hao wa kihistoria wa Uhispania walifungwa 2-1 na Arsenal Jumatano usiku katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa, jambo lililozidi kumweka kikaangoni Ancelotti.

Ingawa Alonso hajarudia mafanikio ya msimu uliopita, Leverkusen kwa sasa wanashika nafasi ya pili katika msimamo wa Bundesliga na walifika hatua ya mtoano Ligi ya Mabingwa Ulaya, kabla ya kutolewa na Bayern Munich.

Mkataba wake na timu hiyo unatarajiwa kumalizika mwaka 2026.