Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Garnacho atua anga za Atletico Madrid

TETESI Pict

Muktasari:

  • Mbali ya Atletico, huduma ya Garnacho pia inahitajika na Bayer Leverkusen na alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kuondoka Januari baada ya kocha Ruben Amorim kuweka wazi kwamba yeye na Rashford hawakuwa wakifanya vile ambavyo yeye alikuwa akielekeza.

ATLETICO Madrid ipo tayari kuweka mezani kiasi cha Pauni 70 milioni kwenda Manchester United kwa ajili ya kuipata saini ya winga wa timu hiyo na Argentina, Alejandro Garnacho, 20.

Mbali ya Atletico, huduma ya Garnacho pia inahitajika na Bayer Leverkusen na alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kuondoka Januari baada ya kocha Ruben Amorim kuweka wazi kwamba yeye na Rashford hawakuwa wakifanya vile ambavyo yeye alikuwa akielekeza.

Tangu kuanza kwa msimu huu, Garnacho amecheza mechi 50 za michuano yote na kufunga mabao 20 na mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.

Licha ya timu nyingi kuhitaji huduma yake, Garnacho haonekani kuwa tayari kuondoka kwa sababu ameshaanza kuaminiwa na Amorim ambaye amekuwa akimpa nafasi kubwa ya kucheza.


Rayan Cherki

MANCHESTER United na Liverpool zipo kwenye vita kali kumwania mshambuliaji wa Olympique Lyon na timu ya taifa ya Ufaransa, Rayam Cherki ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2026. Cherki ameonyesha kiwango bora tangu msimu huu uanze na amefunga mabao 12 katika mechi 39 za michuano yote.



Kingsley Coman

ARSENAL wameanza mazungumzo na wawakilishi wa winga wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Ufaransa, Kingsley Coman, mwenye umri wa miaka 28, wanayehitaji kumsajili dirisha la majira ya kiangazi mwaka huu. Licha ya kuhusishwa na timu mbalimbali za nje ya Ujerumani, ripoti pia zinadai Bayern inapambana kumsainisha mkataba mpya.


Kaua Santos

MANCHESTER United na Tottenham zimefanya mazungumzo na Eintracht Frankfurt kuhusu uwezekano wa kuipata saini ya kipa wa timu hiyo wa kimataifa wa Brazil, Kaua Santos ambaye  anaweza kuuzwa kwa kiasi kisichopungua Pauni 30 milioni.

Santos mwenye umri wa miaka 22, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2030.


Erling Haaland

RAIS wa Real Madrid, Florentino Perez anahitaji huduma ya mshambuliaji wa Manchester City na timu ya taifa ya Norway, Erling Haaland, 24, dirisha lijalo ili kuboresha zaidi eneo lao la ushambuliaji. Perez anamwangalia Haaland kama mbadala sahihi wa Vinicius Jr ambaye muda wowote anaweza akaondoka kwenda Saudi Arabia. Mkataba wa Haaland unamalizika mwaka 2034.


Joao Felix

MSHAMBULIAJI wa Chelsea na timu ya taifa ya Ureno, Joao Felix ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo AC Milan, inadaiwa ana mpango wa kwenda Saudi Arabia mwisho wa msimu huu na ikishindikana atarudi Ureno kujiunga na Benfica. Felix  amepokea ofa nono kutoka timu za Saudia baada ya hivi karibuni kudaiwa kuwa anataka kuondoka Chelsea na kurudi Ureno.


Callum Hudson-Odoi

NOTTINGHAM Forest wapo katika mchakato wa kuanzisha mazungumzo na winga wao wa kimataifa wa England, Callum Hudson-Odoi wanayehitaji kumsainisha mkataba mpya wakati ule wa sasa ukitarajiwa kumalizika mwaka 2028. Odoi mwenye umri wa miaka 24, ni mmoja wa mastaa tegemeo wa kikosi cha kwanza cha Forest na msimu huu amefunga mabao matano.


Georginio Rutter

CHELSEA wanafuatilia kwa karibu maendeleo ya mshambuliaji wa Brighton na Ufaransa, Georginio Rutter ambaye inataka kumsajili katika dirisha la majira ya kiangazi. Rutter ameingia kwenye rada za Chelsea baada ya msimu huu kuonyesha kiwango bora akicheza mechi 34 za michuano yote na kufunga mabao nane.