Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Howe azuia dili la Isak kwa vigogo Ulaya

Muktasari:

  • Isak ambaye anawindwa na vigogo kibao Ulaya ikiwemo Barcelona, Arsenal na Liverpool amekuwa katika kiwango bora tangu msimu uliopita.

KOCHA wa Newcastle United, Eddie Howe amewaambia mabosi kwamba anahitaji kuendelea kuipata huduma ya straika wa kimataifa wa Sweden, Alexander Isak anayehusishwa kuondoka mwisho wa msimu huu.

Isak ambaye anawindwa na vigogo kibao Ulaya ikiwemo Barcelona, Arsenal na Liverpool amekuwa katika kiwango bora tangu msimu uliopita.

Howe anataka kuendelea na Isak kwa sababu anaamini atakuwa msaada mkubwa msimu ujao katika michuano ya kimataifa ambayo tayari Newcastle imefuzu Uefa Conference League. Mkataba wa sasa wa Isak unamalizika  2028. Tangu kuanza msimu huu amecheza mechi 36 michuano yote na kufunga mara 24.


Dean Huijsen

BOURNEMOUTH wapo tayari kumuuza beki kisiki raia wa Hispania, Dean Huijsen, 20, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ambapo anawindwa na Real Madrid na Bayern Munich. Licha ya vigogo hao kuonyesha nia ya kutaka kumsajili, Huijsen hana mpango wa kuondoka nje ya England na badala yake anataka kusaini na moja kati ya timu za England.


Aaron Ramsdale

MANCHESTER United wanaangalia uwezekano wa kumsajili kipa wa  Southampton, Aaron Ramsdale, mwenye umri wa miaka 26, ambaye ameanza kutafuta timu baada ya Soton kushuka daraja. Mabosi wa Man United wanataka kumsajili staa huyo kutokana na kiwango kibovu cha kipa wao wa sasa Andre Onana. Mkataba wa Ramsdale unatarajiwa kumalizika 2028.


Georginio Rutter

CHELSEA wanafuatilia kwa karibu maendeleo ya mshambuliaji wa Brighton na Ufaransa, Georginio Rutter ambaye wanapiga hesabu za kumsajili katika dirisha la majira ya kiangazi. Rutter ameingia kwenye rada za Chelsea baada ya msimu huu kuonyesha kiwango bora akicheza mechi 34 za michuano yote na kufunga mabao manane.


Thomas Partey

ATLETICO Madrid inafikiria kumsajili kiungo wa Arsenal na timu ya taifa ya Ghana, Thomas Partey, 31, ambaye mkataba wake na Arsenal unamalizika mwisho wa msimu huu. Partey anahusishwa kuondoka Arsenal baada ya timu hiyo kutoonyesha nia ya kutaka kumuongoza mkataba kutokana na majeraha ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakimsumbua.


Liam Delap

LICHA ya kutamani kuipata huduma yake, mshambuliaji wa Ipswich Town, Liam Delap anadaiwa kukataa ofa ya Manchester United inayotaka kumsajili katika dirisha la majira ya kiangazi lijalo. Delap aliingia katika rada za Man United inayohitaji straika lakini amechomoa kwa sababu ya hali ambayo inapitia, hivyo haoni kama atakwenda kukuza kipaji chake. Msimu huu amecheza mechi 34 za michuano yote na kufunga mabao 12.


Tammy Abraham

A Milan inataka kumsainisha mkataba wa kudumu straika wa AS Roma, Tammy Abraham, 27, dirisha lijalo la kiangazi baada ya kuridhishwa na kiwango tangu ajiunge kwa mkopo. Roma nayo inataka kumsainisha mkataba wa kudumu kiungo wa AC Milan na Ubelgiji, Alexis Saelemaekers, 25, ambaye anacheza kwa mkopo katika kikosi chao.


Caoimhin Kelleher

WEST Ham United wanataka kumsajili kipa wa Liverpool na wa Jamhuri ya Ireland, Caoimhin Kelleher, mwenye umri wa miaka 26, katika dirisha la majira ya kiangazi. Kelleher anataka kuondoka Liverpool kwa sababu hapati nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza cha majogoo hao. Mkataba wake wa sasa unamalizika 2026.