Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa AFCON Salah kuipa pigo Liverpool

Muktasari:

  • Liverpool imekuwa muathirika mkubwa wa kupoteza wachezaji muhimu kutokana na ratiba ya michuano ya AFCON inayofanyika kila baada ya miaka miwili ambapo zamani mbali ya Salah ilikuwa ikimkosa pia Sadio Mane.

LIVERPOOL, ENGLAND: LICHA ya kuinjoi maisha ikiwa na staa wake raia wa Misri, Mohamed Salah ambaye msimu huu ndio mchezaji anayeongoza kwa kuchangia mabao mengi zaidi katika kikosi chao, Liverpool itatakiwa kujiandaa na tatizo la kumkosa fundi huyu kwa karibia mechi 10 ifikapo msimu ujao.

Liverpool imekuwa muathirika mkubwa wa kupoteza wachezaji muhimu kutokana na ratiba ya michuano ya AFCON inayofanyika kila baada ya miaka miwili ambapo zamani mbali ya Salah ilikuwa ikimkosa pia Sadio Mane.

Salah alikosa mechi tano msimu uliopita baada ya kwenda Ivory Coast kucheza michuano ya AFCON akiwa na Misri na mbaya zaidi aliumia msuli wa mguu na ikabidi akose mechi nyingine saba.

Michuano ya AFCON ambayo mwaka huu imesogezwa mbele kutoka Januari hadi Februari na kwenda Desemba na Januari ili kupisha mashindano ya Kombe la Dunia la FIFA kwa upande wa klabu, yanaonekana kuwa yataathiri sana timu za EPL ambazo zina mastaa raia wa Afrika ambao timu zao zimefuzu michuano hiyo.

Misri ya Salah ipo katika Kundi B na ina ratiba ya kucheza dhidi ya Zimbabwe Desemba 22, Afrika Kusini kwenye Boxing Day na Angola itakayokuwa mechi yao ya mwisho ya kundi Desemba 29.

Kama timu yenye mafanikio zaidi katika historia ya AFCON, ikiwa na mataji saba, Misri inatarajiwa kufika hatua za mwisho za mashindano hayo. Hatua ya mtoano ya 16 bora inatarajiwa kufanyika kati ya Januari 3 hadi 6, robo fainali zitapigwa kati ya Januari 9 hadi 10, nusu fainali Januari 14, mechi ya nafasi ya tatu Januari 17 na fainali itafanyika Januari 18.

Ingawa bado ratiba ya msimu ujao haijatoka lakini kipindi cha tarehe tajwa hapo juu ni wakati ambao ligi itakuwa imechanganya sana na Salah anatarajiwa kukosa mechi muhimu na kwa mujibu wa ratiba ya AFCON staa huyu anatarajiwa kukosa mechi zisizopungua nane ambazo sita itakuwa ni za Ligi Kuu.