Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha PSG apuuza kona za Arsenal

Muktasari:

  • Mabingwa hao wa Ufaransa watakutana na wapinzani kutoka England katika hatua ya mtoano kwa mara ya tatu mfululizo msimu huu  baada ya awali kucheza dhidi ya Aston Villa na Liverpool katika 16 bora na robo fainali.

PARIS, UFARANSA: KOCHA wa PSG, Luis Enrique amepuuzilia mbali uwezo wa Asenal katika mipira ya kona akisema watajiandaa kuelekea mchezo huo kama wanajiandaa dhidi ya timu zingine. PSG itafanya safari kwenda Emirates wiki ijayo kwa ajili ya kucheza mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mkondo wa kwanza.

Mabingwa hao wa Ufaransa watakutana na wapinzani kutoka England katika hatua ya mtoano kwa mara ya tatu mfululizo msimu huu  baada ya awali kucheza dhidi ya Aston Villa na Liverpool katika 16 bora na robo fainali.

Arsenal na PSG zimewahi kukutana mara moja msimu wa 2016/17 katika hatua ya makundi ambapo michezo miwili yote ilimalizika kwa sare.

Hata hivyo, tangu wakati huo Arsenal imeonekana kuimarika hususan katika mipira ya kutengwa kama kona na faulo ambapo kwa sasa ni miongoni mwa timu tishio linapokuja suala la mipira ya aina hiyo. Licha ya hatari hiyo, Enrique hana wasiwasi.

 “Tutajiandaa kwa njia ileile kama tulivyofanya dhidi ya Liverpool,” alisema Enrique alipoulizwa kuhusu balaa la Arsenal la mipira ya kutengwa.

“Liverpool ni timu ambayo ina uwezo kama wa Arsenal au zaidi. Aston Villa pia walikuwa na uwezo mkubwa katika eneo hilo kama ilivyo kwa timu nyingi za Ligue 1. Hatujiandai kwa kuangalia mipira ya kutengwa, lazima tuwe na ushindani kila mahali.” Hata hivyo, kauli ya Enrique kuhusu uwezo wa mipira ya kutengwa wa Liverpool huenda ikawa imekosa mwelekeo kwani licha ya kuwa na msimu bora sio mfano mzuri wa ustadi katika eneo hilo. Kulingana na WhoScored, Liverpool wamefunga mara sita pekee kutokana na mipira hiyo katika msimu wa 2024/25 tofauti na Arsenal waliofunga mara 13.