Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madrid yampigia simu Klopp

Muktasari:

  • Ancelotti amekuwa na mwaka mgumu kwenye viunga Bernabeu, wakiwa nafasi ya pili katika msimamo wa LaLiga na hawakuanza vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.

MADRID, HISPANIA: KOCHA wa zamani wa Liverpool, Jurgen Klopp, anatajwa kuwa katika mazungumzo na mabosi Real Madrid akiwa ni mmoja kati ya makocha ambao wanaweza kurithi mikoba ya Carlo Ancelotti katika kikosi hicho.

Ancelotti amekuwa na mwaka mgumu kwenye viunga Bernabeu, wakiwa nafasi ya pili katika msimamo wa LaLiga na hawakuanza vizuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.

Kiwango cha timu katika michuano ya kimataifa na ligi kinadaiwa kusababisha vikao vya mara kwa mara tangu kuanza kwa mwaka huu na tayari rais wa Madrid, Florentino Perez ameshafanya uamuzi wa kuachana na Ancelotti ifikapo mwisho wa msimu baada ya kukutana na bodi ya timu.

Awali, mtu aliyekuwa anaonekana kuongoza katika orodha ya makocha wanaoweza kumrithi Ancelotti alitajwa kuwa ni Xabi Alonso lakini sasa Klopp naye ameingia katika orodha.

Alonso aliitumikia Madrid kwa miaka mitano kama mchezaji, akishinda LaLiga mwaka 2012, Copa del Rey mbili, na Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2014.

Hata hivyo, ili kumpata Madrid itatakiwa kutoa pesa nyingi kwa ajili ya kuvunja mkataba wake na Bayer Leverkusen unaotarajiwa kumalizika mwaka 2026.

Hali hiyo imesababisha vigogo hao kumwangalia Klopp ambaye haitahitaji kutoa kiasi kikubwa cha pesa ili kuipata saini yake.

Upande wa Klopp ambaye ameshashinda mataji yote makubwa kwa ngazi ya klabu pia kumwajiri inaonekana kuwa itakuwa ni jambo zuri kwani ana uzoefu wa kutosha katika michuano ya kimataifa.

Alonso alizivutia timu nyingi kubwa baada ya msimu uliopita kuiwezesha Leverkusen kushinda taji la Bundesliga, DFB-Pokal na ikafika pia fainali ya Europa League ambapo walichapika dhidi ya Atalanta.

Klopp aliachana na Liverpool mwisho wa msimu uliopita baada ya kudumu kwa miaka tisa akieleza kuwa anahitaji kupumzika.

Hata hivyo, kwa sasa anafanya kazi kama Mkurugenzi wa Michezo wa Kampuni ya Red Bull ambayo inamiliki timu mbalimbali barani Ulaya.