Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makocha watano ubaoni Tottenham Hotspur

MAKOCHA Pict

Muktasari:

  • Kichapo hicho kwenye mchezo wa Ligi Kuu England kimeifanya timu kuendelea kuwamo kwenye 10 la chini kwenye msimamo huku mashabiki wakionyesha hasira kubwa kwa wachezaji wao.

LONDON, ENGLAND: KOCHA, Ange Postecoglou nyakati ngumu zimeendelea kumwandama huko Tottenham Hotspur na hilo linaweza kumgharimu kibarua chake baada ya kuchapwa na Chelsea, usiku wa Alhamisi.

Kichapo hicho kwenye mchezo wa Ligi Kuu England kimeifanya timu kuendelea kuwamo kwenye 10 la chini kwenye msimamo huku mashabiki wakionyesha hasira kubwa kwa wachezaji wao.

Ushindi huo kwa Chelsea ina maana msimu huu imeshinda nyumbani na ugenini dhidi ya wapinzani wao hao wa London na hiyo Alhamisi huko uwanjani Stamford Bridge, mashabiki wa Spurs walikuwa wakiimba “hujui unachokifanya” wakilenga kumshambulia kocha huyo kwenye benchi lake la ufundi.

Kutokana na hilo, tayari kibarua cha kocha Postecoglou kipo kwenye mashaka makubwa kwa sababu Spurs ipo kwenye hatari ya kumaliza chini zaidi kwenye msimamo wa ligi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 15.

Matokeo ya hivyo yamefanya sasa kuwapo na orodha ya makocha watano wanaohusishwa na kibarua cha kwenda kuinoa Spurs, akiwamo kocha wa zamani wa miamba hiyo, Mauricio Pochettino.

Makocha wengine wanaohusishwa na kibarua hicho cha Spurs ni Marco Silva wa Fulham, Andoni Iraola, ambaye amefanya vizuri huko Bournemouth, Kieran McKenna wa Ipswich Town na Thomas Frank, ambaye amehusishwa na kibarua hicho kizito cha huko London kutoana na kufanya vizuri kwenye kikosi cha Brentford.

Pochettino kwa sasa ni kocha wa timu ya taifa ya Marekani, lakini hilo halimzuii kuhusishwa na mpango wa kurudi kwenye klabu hiyo ya Spurs, ambayo aliwahi kuifikisha fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.