Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United yaachana rasmi na Hojlund akienda Napoli

Muktasari:

  • Mkataba huo umekamilishwa baada ya Napoli kufuzu kwa ajili michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, huku tayari ikiwa imelipa Manchester United Pauni 5.2 milioni za mkopo wa Hojlund msimu huu.

MANCHESTER, ENGLAND: Rasmus Hojlund amekamilisha rasmi uhamisho wa Pauni 38 milioni kutoka Manchester United kwenda Napoli, klabu hiyo imethibitisha.

Mkataba huo umekamilishwa baada ya Napoli kufuzu kwa ajili michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, huku tayari ikiwa imelipa Manchester United Pauni 5.2 milioni za mkopo wa Hojlund msimu huu.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Denmark mwenye umri wa miaka 23, ambaye aliwahi kucheza Italia akiwa na Atalanta kabla ya kuhamia Old Trafford miaka mitatu iliyopita kwa dau lililofikia Pauni 72 milioni aliifungia Napoli mabao 16 baada ya kurejea Serie A.

Hojlund pia alifunga mabao 26 katika mechi 95 alizoichezea Manchester United, lakini alifahamu kuwa nafasi yake ya kucheza ingepungua baada ya klabu hiyo kutumia Pauni 74 milioni kumsajili Benjamin Sesko msimu uliopita.

Taarifa ya klabu imesema: "Rasmus Hojlund amejiunga na Napoli kwa mkataba wa kudumu. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark alitumia msimu uliopita kwa mkopo katika klabu hiyo ya Italia, akifunga mabao 16 katika mechi 44 za mashindano yote, na sasa amejiunga rasmi na klabu ya Naples.

"Shabiki huyo wa Manchester United tangu utotoni alisajiliwa kutoka Atalanta katika majira ya joto ya mwaka 2023 na baadaye akafunga mabao 26 katika mechi 95. Alikuwa sehemu ya kikosi cha Reds kilichonyakua Kombe la FA mwezi Mei 2024 baada ya kuingia kama mchezaji wa akiba dhidi ya Manchester City katika Uwanja wa Wembley.

"Mwanzoni mwa msimu wa 2025-26, Hojlund alirejea Italia kwa mkopo wa msimu mzima, akiisaidia Napoli kushinda Supercoppa Italiana na kumaliza nafasi ya pili katika Serie A. Kila mmoja ndani ya klabu anamtakia Rasmus kila la heri katika siku zijazo."

Uthibitisho wa kuondoka kwa Hojlund umekuja baada ya Manchester United kufikia makubaliano na Atalanta kuhusu usajili wa kiungo wa Brazil Ederson kwa Pauni 38 milioni.

Klabu hiyo pia inatarajia kukamilisha uhamisho wa kudumu wa Marcus Rashford na Andre Onana, ambao walitumia msimu huu kwa mkopo katika timu za Barcelona na Trabzonspor mtawalia.

Mkataba wa Rashford huko Barcelona una kipengele kinachoiruhusu kumnunua kwa Pauni 26 milioni kabla ya Juni 15, ingawa viongozi wa timu hiyo wameonyesha nia ya kulipa karibu nusu ya kiasi hicho au kuomba mkopo mwingine baada ya kutumia Pauni 69.3 milioni kumsajili nyota mwenzake wa timu ya taifa ya England, Anthony Gordon.

Kwa upande wa Onana, Trabzonspor wanataka kumbakiza, lakini ada ya uhamisho na mshahara wake vinaweza kufanya mkopo mwingine wa msimu mmoja kuwa chaguo linalowezekana zaidi.