Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbappe ampiku Ronaldo, amfukuzia Ronaldo

MBAPPE Pict

Muktasari:

  • Mbappe alifunga mabao mawili katika dakika sita  katika mechi hiyo alifanikiwa kuivuka rekodi ya Ronaldo kwa idadi ya mabao.

MADRID, HISPANIA: STRAIKA wa Real Madrid, Kylian Mbappe ameivunja rekodi ya kufunga mabao mengi katika mashindano yote msimu mmoja iliyokuwa ikishikiliwa na Ronaldo De Lima nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil katika historia ya klabu hiyo.

Mabao mawili ndani ya dakika sita aliyoyafunga juzi Jumamosi kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Villarreal wa Ligi Kuu ya Hispania, La Liga, yalimfanya afikishe mabao 31 na kumpita Ronaldo De Lima mwenye 30 aliyoiweka msimu wa 2002/03.

Hata hivyo, Mbappe ana mtihani wa kuifikia na kuivunja rekodi ya nyota wa zamani wa klabu hiyo Ivan Zamorano mwenye mabao 37 aliyefanya hivyo msimu wa 1992/93 na sasa amebakiza mabao sita msimu huu kuifikia.

Kabla ya kuifikia rekodi hiyo, Mbappe ana mtihani mwingine wa kuifikia na kuivunja rekodi ya Cristiano Ronaldo aliyoiweka msimu wa 2009/10 na Ruud Van Nistelrooy 2006/07 ambao wana mabao 33 katika msimu wao wa kwanza walipojiunga na timu hiyo.

Mbappe ambaye ndiyo msimu wake wa kwanza Madrid akitokea Paris Saint Germain ya Ufaransa, hakuanza na moto ingawa sasa amekuwa na msimu mzuri na anakuwa pia mchezaji wa nne kufunga mabao mengi katika msimu wa kwanza.

Tangu kuanza kwa mwaka huu Mbappe ndio anaonekana kuimarika zaidi na rekodi zinaonyesha anashikilia nafasi ya pili katika orodha ya wachezaji waliofunga mabao mengi zaidi katika ligi tano bora barani Ulaya akizidiwa na Ousmane Dembele pekee mwenye 21 na Mbappe 17.

Katika ligi, Mbappe mwenye mabao 20 hadi sasa amezidiwa na Robert Lewandowski mwenye mabao 21 na kuifanya vita ya ufungaji kuwa tamu huku wa tatu ni Ante Budimir mwenye 14, kabla ya mechi za jana na Barcelona ilikuwa ugenini dhidi ya Atletico Madrid.