Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbappe: Wale kina Ronaldo ni magwiji

Muktasari:

  • Mbappe, hakutaka kabisa kulinganishwa na mshindi huyo mara tano wa Ballon d'Or.

MADRID, HISPANIA: STAA wa Real Madrid, Kylian Mbappe amekataa kulinganishwa na supastaa Cristiano Ronaldo baada ya kukaribia kuipiku rekodi ya mabao ya mkali huyo wa Ureno katika msimu wake wa kwanza na miamba hiyo ya Bernabeu.

Mbappe, hakutaka kabisa kulinganishwa na mshindi huyo mara tano wa Ballon d'Or.

Mbappe sasa amefunga mabao 30 katika mechi 43 alizochezea Real Madrid kwenye michuano yote.

Mabao yake mawili aliyofunga kwenye ushindi wa 2-1 dhidi ya Villarreal, umezidi kunogesha rekodi za mshambuliaji huyo wa Les Bleus katika msimu wake wa kwanza katika kikosi hicho kinachonolewa na Mtaliano, Carlo Ancelotti.

Lakini, mabao hayo yalimfanya Mbappe kuvunja rekodi ya Ronaldo Nazario katika msimu wake kwanza katika klabu hiyo ya Hispania.

Baada ya kusajiliwa kutoka Inter Milan mwaka 2002, Ronaldo wa Brazil alifunga mabao 29 katika mechi 43. Huku mabao yake hayo yaliisaidia Los Blancos kushinda ubingwa wa La Liga, ikimaliza ligi pointi mbili juu ya Real Sociedad.

Na sasa, Mbappe amebakiza mabao matatu tu kumfikia Ronaldo wa Ureno katika msimu wake kwanza Santiago Bernabeu.

Akizungumza baada ya mechi hiyo, Mbappe, 26, aliulizwa kuhusu kuvuka rekodi ya Ronaldo de Lima na kufukuzia rekodi ya CR7, alisema: "Hao ni magwiji ambao walikuwa na zama zao. Ni kitu muhimu, lakini hilo ni suala la namba. Kama nitafunga mabao mengi kuliko Ronaldo na Cristiano, hiyo haina maana kuwa mimi ni mkubwa, huu ndiyo kwanza ni msimu wangu wa kwanza.

"Kitu muhimu ni kuisaidia timu kushinda mataji. Kufunga ni jambo muhimu, lakini yatakuwa muhimu zaidi kama tutashinda La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Copa del Rey."

Ronaldo wa Ureno alijiunga na Real Madrid kwa ada uliyoweka rekodi ya dunia wakati aliponaswa kutoka Manchester United mwaka 2009 kwa Pauni 80 milioni. Alifunga mabao 33 katika mechi 35 katika msimu wake wa kwanza. Hata hivyo, msimu huo, Madrid haikushinda taji lolote, ambapo timu hiyo ilimaliza pointi tatu nyuma ya mahasimu wao, Barcelona.

Mbappe, kwa upande wake bado ana nafasi ya kushinda mataji matatu msimu huu baada ya kikosi hicho kutinga pia kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kwenye La Liga ipo vizuri na kwenye Copa del Rey ipo nusu fainali na ilishinda 1-0 kwenye mechi yake ya kwanza dhidi ya Real Sociedad, hivyo inasubiri mechi ya marudiano mwezi ujao. Kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya itakipiga na Arsenal.

MABAO MENGI KWENYE MSIMU WA KWANZA  REAL MADRID

1.Cristiano Ronaldo, mabao 33

2.Ruud van Nistelrooy, mabao 33

3.Kylian Mbappe, mabao 31

4.Ronaldo Nazario, mabao 30

5.Jude Bellingham, mabao 23