Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mikel Obi afichua usajili wa Osimhen

OBI Pict

Muktasari:

  • Osimhen, ambaye amekuwa akihusishwa na uhamisho kwenda England kwa muda mrefu, alikuwa karibu kujiunga na Chelsea katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana, lakini dili lilifeli katika dakika za mwisho na badala yake akatua Galatasaray kwa mkopo.

LONDON, ENGLAND: RAFIKI wa Victor Osimhen ambaye ni mchezaji wa zamani wa Chelsea, John Obi Mikel amesema staa huyo anatamani na anataka kucheza Chelsea licha ya tetesi zinazodai kwamba yupo karibu kutua Manchester United.

Osimhen, ambaye amekuwa akihusishwa na uhamisho kwenda England kwa muda mrefu, alikuwa karibu kujiunga na Chelsea katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana, lakini dili lilifeli katika dakika za mwisho na badala yake akatua Galatasaray kwa mkopo.

Akiwa huko Uturuki, Osimhen ameendeleza kiwango cha juu, akifunga mabao 31 katika mechi 36, na Napoli wapo tayari kumwachia katika dirisha hili.

Chelsea bado wanatafuta mshambuliaji namba tisa, baada ya kocha wao Enzo Maresca kutoridhishwa sana na kiwango cha Nicolas Jackson.

Akizungumza na beIN Sports, gwiji huyo wa Chelsea alisema: "Anataka kuchezea Chelsea. Natumai atasaini hapo. Najua tulipoishia kwenye mazungumzo ya mkataba, najua tulipo. Ni suala rahisi tu, kwa sababu kazi kubwa tulifanya katika dirisha la majira ya kiangazi lililopita. Ni rahisi kuendeleza pale dili lilipoishia.

"Huyu jamaa anachojua kufanya ni kufunga mabao, kitu ambacho tumekikosa msimu huu, hatufungi vya kutosha na ndio maana tuko hapa tulipo."

Obi anadaiwa kuwa mmoja kati ya watu waliohusika kwenye mazungumzo ya Osimhen kutua Chelsea katika dirisha lililopita na aliwahi kusema pia mwaka jana kwamba kulikuwa na mambo madogo ambayo yalichangia dili hilo kutokamilika na ilishindikana kwa sababu muda wa dirisha pia ulishaisha.