Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mo Salah, Van Dijk vikumbo kwenye tuzo

VIKUMBO Pict

Muktasari:

  • Liverpool imenyakua ubingwa wa Ligi Kuu England ikiwa ni msimu wa kwanza kwa kocha wao mpya Arne Slot, ambaye pia amewekwa kuwania tuzo ya Kocha Bora wa Msimu.

LONDON, ENGLAND: MASTAA wa wanane wamewekwa kwenye orodha ya wakali wanaowahia tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu kwenye Ligi Kuu England msimu huu, hukuu Liverpool ikiwakilishwa na wachezaji watatu.

Liverpool imenyakua ubingwa wa Ligi Kuu England ikiwa ni msimu wa kwanza kwa kocha wao mpya Arne Slot, ambaye pia amewekwa kuwania tuzo ya Kocha Bora wa Msimu.

Wachezaji hao watatu wa kutoka Merseyside watakaowania kwenye tuzo hiyo ya Mchezaji Bora wa Mwaka ni Ryan Gravenberch, Mohamed Salah na Virgil van Dijk. Gravenberch alionyesha kiwango bora akicheza Namba 6 mwanzo mwisho baada ya kukwama kwa usajili wa Martin Zubimendi.

Van Dijk kwa upande wake amekuwa kwenye kiwango bora kabisa akiweka rekodi ya kuwa nahodha wa kwanza wa Kidachi kuongoza timu kushinda ubingwa wa Ligi Kuu England. Na Salah amekuwa gumzo kubwa, akifunga mabao 28 na kuasisti 18 kwenye ligi hiyo msimu huu.

Mastaa hao watatu wa Liverpool wataingia kwenye vita kubwa na wachezaji wengine watano. Staa wa Manchester City, Phil Foden alishinda mwaka jana, lakini hakuna mchezaji yeyote aliyepenya kwenye tuzo za mwaka huu kutoka kwenye kikosi cha Pep Guardiola.

Mchezaji wa Arsenal, aliyeingia kwenye kinyang'anyiro hicho ni kiungo wao ghali, Declan Rice baada ya kuonyesha kiwango bora kabisa kwenye kikosi hicho cha Emirates. Wengine wanaowania tuzo hiyo ni staa wa Nottingham Forest, Morgan Gibbs-White - ambapo kiungo huyo alikuwa sehemu muhimu ya kikosi hicho katika kufukuzia tiketi ya kucheza michuano ya Ulaya baada ya miaka 30.

Gibbs-White ataungana na mchezaji mwenzake Chris Wood na straika huyo wa miaka 33 amefunga mabao 20 ikiwa msimu wake bora kabisa. Akitajwa kushiriki tena msimu huu ni straika wa Newcastle United, Alexander Isak, ambaye amefunga mabao 23 na kuwamo kwenye mbio za kufukuzia Kiatu cha Dhahabu cha Ligi Kuu England. Jina la mwisho kwenye orodha hiyo ni Bryan Mbeumo, na winga huyo wa Brentford akifunga mabao 18 na kuasisti mara saba.

Kwa upande wa makocha watakaowania tuzo ni Slot, Thomas Frank wa Brentford, Eddie Howe wa Newcastle, Nuno Espirito Santo wa Nottingham Forest na Vitor Pereira wa Wolves.

Kinda Bora wa Mwaka tuzo hiyo itawaniwa na Gravenberch (Liverpool), William Saliba (Arsenal),

Anthony Elanga (Nottingham Forest), Cole Palmer (Chelsea), Liam Delap (Ipswich Town), Joao Pedro (Brighton), Morgan Rogers (Aston Villa) na Dean Huijsen (Bournemouth).