Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rashford aitaka Ligi ya Mabingwa Ulaya

RASHFORD Pict

Muktasari:

  • Rashford ambaye amekuwa na kiwango kizuri Villa akifunga bao lake la nne tangu ajiunge nao katika kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Manchester City, inaelezwa pia hana mpango wa kubaki Villa Park na anahusishwa kwenda Hispania.

MANCHESTER, ENGLAND: MSHAMBULIAJI wa Manchester United anayekipiga kwa mkopo Aston Villa, Marcus Rashford ameanza kutafuta timu nje ya England baada ya kuona hawezi kurudi Old Trafford mwisho wa msimu na anataka kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Rashford ambaye amekuwa na kiwango kizuri Villa akifunga bao lake la nne tangu ajiunge nao katika kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Manchester City, inaelezwa pia hana mpango wa kubaki Villa Park na anahusishwa kwenda Hispania.

Inaelezwa pia kurejea kwa nyota huyo wa England Man United ni ngumu kutokana na Kocha Ruben Amorim kusema hamhitaji tena, ingawa mkataba wake na miamba hiyo unamalizika mwaka 2028.

Vyanzo vya karibu na Rashford vimeiambia tovuti ya The Mirror  kuwa mshambuliaji huyo hataki kujiunga na timu yoyote ya Jiji la London, lakini anatamani kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, huku Villa ikipoteza matumaini ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao baada ya kichapo kutoka kwa City.

Hivyo, Rashford (27), hatma yake itafahamika mwisho wa msimu ingawa na mwenyewe alishasema anataka kucheza timu inayoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya na hataki kucheza England, licha ya Villa ilikuwa na chaguo la kumsainisha mkataba wa kudumu kwa kutoa Pauni 40 milioni.

Pia wawakilishi wa Rashford pia wamekanusha uwezekano wa staa huyo kutumika na Man United kama sehemu ya mpango wa kubadilishana wachezaji ili kuwapata Ollie Watkins wa Villa au Eberechi Eze.