Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo nahodha gemu ya Messi

RIYADH, SAUDI ARABIA. CRISTIANO Ronaldo ameriporiwa mechi yake ya kwanza atakayocheza huko Saudi Arabia atakabidhiwa kitambaa cha unahodha wakati atakapokabiliana na mpinzani wake wa siku nyingi Lionel Messi.

Ronaldo na Messi wamekuwa kwenye upinzani mkali kwa zaidi ya miaka 15. Wawili hao walikuwa wakipokezana tu tuzo ya Ballon d'Or kati ya 2008 na 2017.

Lakini, kwa sasa Ronaldo ameachana na soka la Ulaya baada ya kujiunga na Al Nassr ya Saudi Arabia kufuatia kusitishiwa mkataba wake Manchester United.

Kwenye dili hilo la Al Nassr, Ronaldo atalipwa Pauni 173 milioni kwa mwaka na sasa mechi yake ya kwanza atakabiliana na Paris Saint-Germain ya Messi kwenye mechi ya kirafiki kesho Alhamisi.
Mastaa wa Al Nassr na Al Hilal wataunda kikosi kimoja kitakachochuana na PSG, ambapo Ronaldo atakutana na Messi.

Na kinachoripotiwa kwa sasa huenda Messi na Ronaldo wakachuana sana kwenye soka la Saudi Arabia baada ya kuwapo na ripoti kwamba supastaa huyo wa Argentina ametengewa mkwanja mrefu na miamba ya Al Hilal ikihitaji huduma yake.

Wiki iliyopita, vyombo vya habari za Saudi Arabia viliripoti kwamba baba yake Messi alionekana huko Riyadh akijadili juu ya ofa hiyo. Licha ya hilo, Messi amekuwa akiripotiwa kufikia makubaliano ya mdomo na PSG juu ya kuongeza mkataba zaidi wa kubaki kwenye kikosi hicho cha miamba ya Ufaransa.