Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Salah aibu! aweka rekodi mbaya Carabao Cup

Muktasari:

  • Katika mchezo huo, Liverpool ilikubali kipigo cha mabao 2-1.

LONDON, ENGLAND: SUPASTAA, Mohamed Salah ametengeneza rekodi mbaya kabisa kwenye mechi aliyoshuhudia timu yake ya Liverpool ikikumbana na kipigo kutoka kwa Newcastle United kwenye fainali ya Kombe la Ligi, uwanjani Wembley.

Katika mchezo huo, Liverpool ilikubali kipigo cha mabao 2-1.

Licha ya Federico Chiesa kufunga kwenye dakika za mwisho, mabao ya Dan Burn na Alexander Isak yalitosha kuifanya Newcastle kubeba taji lake la kwanza la michuano ya ndani baada ya miaka 70.

Salah, ambaye amefunga mabao 32 msimu huu, alianzishwa na kocha Arne Slot akiamini kwamba ataendeleza moto wake wa kupachika mabao. Lakini, mkali huyo wa kimataifa wa Misri, hakuwa na maajabu yoyote kwa muda wote aliocheza akitokea wingi ya kulia.

Na si tu Salah alishindwa kufunga bao kwenye mechi hiyo, bali hata shuti moja kulenga goli hakupiga na alishindwa kutengeneza nafasi kwa ajili ya wachezaji wenzake kwa dakika zote 90 alizokuwa ndani ya uwanja.

Hiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Salah katika maisha yake kwenye kikosi cha Liverpool kushindwa kufanya lolote katika mechi. Alifanikiwa walau kufanya moja kati ya kufunga, kuasisti au kupiga shuti kulenga goli katika mechi 391 alizochezea timu hiyo tangu aliponaswa na miamba hiyo ya Anfield mwaka 2017.

Beki wa zamani wa Manchester United na mchambuzi wa soka, Gary Neville alishangazwa na namna Salah alivyoshindwa kabisa kuonyesha makali katika mechi hiyo, aliposema: "Sijawahi kumwona Mo Salah akiwa kimya hivi kama ilivyo kwenye mechi hii. Amegusa mpira mara tatu tu kwenye dakika 25 za kipindi cha pili."

Na sasa, Mo Salah ameshindwa kufunga kwenye mechi mfululizo baada ya kutoka kapa katikati ya wiki, wakati miamba hiyo ilipotupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na miamba ya soka ya Ufaransa, Paris Saint-Germain.

Hata hivyo, alifunga mkwaju wake wa penalti kwenye hatua ya kupigiana matuta baada ya dakika 120. Mkataba wa staa huyo utafika tamati mwishoni mwa msimu huu na bado hakuna maelezo yoyote kama atasaini dili jipya la kuendelea kubaki Anfield.

Mo Salah katika msimu huu, amefunga mabao 32 na kuasisti 22 katika mechi 43 alizocheza kwenye michuano yote.