Sane akataa kurudi England

Muktasari:
- Sane ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu, timu kibao za England na Hispania mbali ya Arsenal Liverpool zinatamani sana saini yake kwa muda mrefu zikiamini gharama itakuwa ndogo kwa kumpata bure.
MUNICH, UJERUMANI: WINGA wa Bayern Munich ambaye anawindwa na timu mbalimbali za England ikiwemo Arsenal na Liverpool anadaiwa kufanya uamuzi wa kusalia timu hiyo kwa msimu ujao ambapo atasaini mkataba wa muda mrefu.
Sane ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu, timu kibao za England na Hispania mbali ya Arsenal Liverpool zinatamani sana saini yake kwa muda mrefu zikiamini gharama itakuwa ndogo kwa kumpata bure.
Hilo huenda lisifanikiwe kwani taarifa kutoka tovuti ya Sky Germany zinaeleza, Sane amepewa ofa ya mkataba mpya na Bayern utakaomwezesha kukaa hadi msimu wa majira ya kiangazi mwaka 2028.
Hata hivyo, mkataba huo umekuja na punguzo kubwa la mshahara kutoka Euro 20 milioni kwa mwaka anaoupata sasa hadi Euro 10 milioni ambayo inaweza kuongeza kufikia Euro 15 milioni ikiwa ataonyesha kiwango bora.
Licha ya punguzo hilo ripoti zimesema kuwa Sane yuko tayari kubaki Bayern baada ya msimu huu na hatofungua milango ya kurudi Ligi Kuu England wala kwenda kwingineko.
Bayern kwa taratibu wanakaribia kushinda taji la Bundesliga msimu huu na pia wana nafasi ya kushinda Ligi ya Mabingwa.