Scholes aungana na Matic kumsema Onana

Muktasari:
- Onana aliingia katika mvutano mkali wa maneno na Matic, kabla ya mechi ya Europa League dhidi ya Lyon usiku wa juzi ambapo Matic alisema kipa huyu ni moja kati ya makipa wenye viwango vya chini kuwahi kutokea katika kikosi cha Man United.
MANCHESTER, ENGLAND: KIUNGO wa zamani wa Manchester United, Paul Scholes ameungana na kiungo wa Olympique Lyon ambaye amewahi kucheza katika viunga vya Old Trafford, Nemanja Matic katika kukosoa kiwango cha kipa Andre Onana anayewatumikia mashetani hao wekundu.
Onana aliingia katika mvutano mkali wa maneno na Matic, kabla ya mechi ya Europa League dhidi ya Lyon usiku wa juzi ambapo Matic alisema kipa huyu ni moja kati ya makipa wenye viwango vya chini kuwahi kutokea katika kikosi cha Man United.
Onana alijibu kwa kusema "angalau nimeshinda kombe" kiti ambacho Matic hakuwahi kushinda katika maisha yake ndani ya Man United.
Na wawili hao walikutana hatimaye Alhamisi katika mchezo wa robo fainali ya Europa uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.
Onana alifanya makosa makubwa yaliyozalisha mabao yote ya Lyon, ikiwemo goli la dakika za jioni la kusawazisha lililofungwa na..
Matic aliketi kwenye benchi akiwa sio sehemu ya wachezaji waliocheza mechi hiyo lakini bila shaka alijiona kuwa mshindi juu ya maoni yake.
Akizungumza kwenye TNT Sports, Scholes, alimkosoa vikali Onana juu ya bao la kwanza la Lyon akisema:"Labda Onana angenyamaza kwanza kabla ya mechi. Amefanya kosa kubwa sana ni kweli mpigaji alipiga vizuri lakini sidhani kama kipa anajua anachofanya. Ni kosa kubwa kutoka kwake."
Mwisho wa mechi, Scholes aliendelea na mashambulizi dhidi ya Onana, akiongeza:
"Nadhani Onana alikuwa na makosa makubwa kwa goli la kwanza, najua ilikuwa ngumu lakini alipaswa kufanya bora zaidi kuliko hivyo alivyofanya."