Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Slot afichua siri ya Mohamed Salah

SLOT Pict

Muktasari:

  • Salah alianza msimu kama mshindani mkubwa wa kushinda kiatu cha dhahabu na tuzo nyingine kubwa barani Ulaya baada ya kuiongoza Liverpool katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu na pia kuisaidia kumaliza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa ikiwa kileleni.

LIVERPOOL, ENGLAND: KOCHA wa Liverpool, Arne Slot, amefichua siri ya kinachosababisha ukame wa mabao wa staa wake, Mohamed Salah katika kipindi cha hivi karibuni. 

Salah alianza msimu kama mshindani mkubwa wa kushinda kiatu cha dhahabu na tuzo nyingine kubwa barani Ulaya baada ya kuiongoza Liverpool katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu na pia kuisaidia kumaliza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa ikiwa kileleni.

Hata hivyo, tangu wakati huo, Liverpool wameondolewa katika mashindano ya Ulaya na FA Cup, na pia walipoteza katika fainali ya Kombe la Carabao. 

Hali ya Salah kama mchezaji tegemeo ambaye alikuwa akipewa nafasi pia ya kushinda Ballon D'or ijayo imekuwa finyu, huku wachezaji wa Barcelona, Raphinha na Lamine Yamal, pamoja na Kylian Mbappe wa Real Madrid, wakionyesha kiwango cha juu kilichodumu hadi sasa.

Zaidi ya hayo, Salah ameshindwa kufunga katika michezo yake minne iliyopita na hakufunga bao lolote lisilo la mpira wa kutengwa tangu Februari 24.

Akizungumza na waandishi wa habari, Slot alisema: "Wakati mwingine ratiba ya mechi ni ngumu zaidi kuliko vipindi vingine. PSG ni moja ya timu bora barani Ulaya kwa sasa. Newcastle walikuwa wakizunguka sana kwenye fainali ya Carabao na Everton walikuwa wagumu sana kufunguka, walikuwa na wachezaji 10 kwenye boksi lao kila wakati.

"Najua Mo, yeye anaishi kwa ajili ya mabao. Ingekuwa ajabu kama angekuwa na furaha kwa kutofunga, sifa yake kubwa huwa anaweza akacheza mchezo mbaya lakini bado akafunga, anapitia kipindi kigumu kwa sasa lakini hii sio kwake tu, huwa inawatokea wachezaji wengine pia."

Licha ya kutofunga katika mechi hizo nne, Salah bado ameendelea kuongoza katika orodha ya wafungaji bora wa EPL akiwa na mabao 27, pia ana nafasi ya kushinda medali ya ubingwa wa ligi akiwa na Liverpool ambayo ndio inaongoza msimamo kwa sasa.