Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Thunder vs Nuggets Mambo manne moto 'game 7'

Muktasari:

  • Nuggets na Thunder zimepigana kiume kwenye mechi sita za nusu fainali ya Ukanda wa Mashariki, lakini hakuna aliyeweza kumtoa mwenzake. Sasa mchuano wa saba ndiyo wa kuamua hatima yao, kwenye mechi ya mwisho ya dakika 48 (au zaidi endapo kutakuwa na muda wa nyongeza).

OKLAHOMA, MAREKANI: MUDA umefika wa kufa na kupona.Ni Jumapili hii, ambapo kila kitu kipo mezani wakati ambao Denver Nuggets na Oklahoma City Thunder watakuwa wakipigania fursa ya kusonga mbele kwenye NBA.

Nuggets na Thunder zimepigana kiume kwenye mechi sita za nusu fainali ya Ukanda wa Mashariki, lakini hakuna aliyeweza kumtoa mwenzake. Sasa mchuano wa saba ndiyo wa kuamua hatima yao, kwenye mechi ya mwisho ya dakika 48 (au zaidi endapo kutakuwa na muda wa nyongeza).

Hii ni mara ya kwanza kwa kikosi hiki cha sasa cha Thunder kucheza game 7, tofauti na Nuggets ambayo ina uzoefu mkubwa imecheza game 7 mara nyingi zaidi kuliko timu yoyote katika miaka saba iliyopita, ikiwa na rekodi ya ushindi wa mechi nne kati ya sita.

Kocha wa muda wa Nuggets, David Adelman, amesema: “Kila mchezo ni hadithi mpya, una maisha yake.”


1. DABI YA MVP: JOKIĆ vs SHAI

Nikola Jokic (Nuggets) na Shai Gilgeous-Alexander (Thunder) wanapambana ndani ya game 7, huku tuzo ya Mchezaji Bora wa Msimu (MVP) ikiwa bado haijatangazwa japo kura tayari zilishapigwa. Ingawa ni tuzo ya msimu wa kawaida - mchezo huo unaweza kuwa tamati ya majibizano kati ya wawili hao waliozibeba timu zao.

Kwa Jokic: Ana kazi ya kuwavuka akina Chet Holmgren, Isaiah Hartenstein na Jalen Williams kizuizi kilichomchosha kwa sehemu kubwa ya mfululizo huu. Je, ataweza kufika robo ya mwisho akiwa bado na nguvu?

Kwa Shai: Atajua lini apige shuti na lini asambaze mpira? Na je, atapewa faulo za kutosha na waamuzi anapojaribu kupenya ngome ya wapinzani? Jibu la maswali haya linaweza kuamua mshindi wa mechi hii.


2. AFYA YA GORDON

Mwishoni mwa game 6, Aaron Gordon alionekana kushika mguu wake wa kushoto ishara kuwa msuli wa paja (hamstring) ni tatizo. Licha ya kuwa na siku mbili za mapumziko, haitoshi kwa aina hii ya majeraha ambayo huhitaji wiki kupoa.

Gordon ni mhimili wa Nuggets, ameshinda mechi mbili kwa mashuti ya mwisho na kusaidia kupeleka moja hadi muda wa nyongeza. Ikiwa hataweza kucheza kikamilifu, Nuggets watahitaji kumtegemea mchezaji ambaye hana uzoefu mkubwa katika mechi kubwa kama hii. Zaidi ya hapo, Michael Porter Jr bado anasumbuliwa na bega na amefunga pointi 3 au pungufu kwenye mechi tatu kati ya sita. Kwa hali hiyo, presha ya ushambuliaji itazidi.


3. WESTBROOK NA UKURASA MPYA

Russell Westbrook amerudi OKC jiji alilowahi kulimiliki kama mfalme, aliposhinda tuzo ya MVP. Lakini katika mfululizo huu akiwa na Nuggets. Thunder wanamdharau kwa kumwacha apige mashuti kwa uhuru na anaendelea kushindwa kutumia nafasi hiyo. Ana asilimia 18 ya mafanikio kwenye mashuti ya mbali na 35% kwa ujumla. Katika mechi tatu zilizopita, ametupa mipira mingi zaidi kuliko alivyofunga.

Licha ya hivyo, Westbrook bado ana nguvu na roho ya kupambana. Lakini pia ana kasumba ya kurudi polepole kwenye ulinzi baada ya kufanya makosa. Game 7 ni nafasi yake ya mwisho na kufanya hivyo katika jiji alilotoka.


4. BENCHI LA OKC

Nguvu ya Thunder msimu huu iko kwenye upana wa kikosi. Iwapo nyota kama Jalen Williams au Lu Dort watakuwa na siku mbaya, bado Thunder inaweza kubaki imara kutokana na nguvu ya benchi. Lakini Jalen Williams  anayetarajiwa kuwa mchezaji wa pili kwa uzito baada ya Shai amekuwa na mechi mbovu mfululizo: 5/20, 5/14, 3/16 na 2/13 kwa mashuti. Je, kocha Mark Daigneault atamvumilia kwa muda gani akianza vibaya game 7?

Thunder wana chaguo la kuwategemea vijana walioko benchi kama Cason Wallace au Aaron Wiggins ambao wamefanya vizuri wanapoitwa uwanjani. Muda wa mapumziko hautakuwepo kila dakika ni muhimu.