Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wakufunzi watano freshi Arsenal

WAKUFUNZI Pict

Muktasari:

  • Arteta alisaini mkataba mpya Septemba mwaka jana, lakini timu yake ya makocha ilikuwa inakaribia kuona mikataba yao ikimalizika mwisho wa msimu huu.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL imefikia makubaliano ya kuwasainisha mikataba mipya wakufunzi watano ambao ni sehemu ya benchi lao la ufundi chini ya kocha Mikel Arteta.

Arteta alisaini mkataba mpya Septemba mwaka jana, lakini timu yake ya makocha ilikuwa inakaribia kuona mikataba yao ikimalizika mwisho wa msimu huu.

Kocha huyu aliajiriwa na kundi lake la makocha watano tangu alipojiunga na Arsenal, Desemba 2019 ambao ni pamoja na makocha wasaidizi Albert Stuivenberg na Carlos Cuesta, kocha wa timu ya kwanza Miguel Molina, kocha wa makipa Inaki Cana, na mtaalamu wa mipira ya kona Nicolas Jover.

Arteta alisaini mkataba wake wa muda mrefu mwaka jana, kumuweka Emirates hadi katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka 2027.

Wasaidizi hawa na Arteta waliiwezesha Arsenal kushinda Kombe la FA mwaka 2020, pamoja na kumaliza mara mbili katika nafasi mbili za juu katika Ligi Kuu England.

Stuivenberg alijiunga na Arsenal wakati Arteta alipoanza kazi na amekuwa akiaminika sana na Arteta, na mara kadhaa ambazo Arteta amekuwa akikumbwa na adhabu, huyu ndio amekuwa akisimama kama kocha. Cana yeye pia alijiunga na Arsenal  wakati Arteta alipotua ingawa yeye alitokea Brentford kama kocha wa makipa.

Cuesta na Molina walitua majira ya kiangazi mwaka 2020 wakati mtaalamu wa mipira ya kutengwa Jover anayesifika sana kwa kuibadilisha timu linapokuja suala la mipira ya aina hiyo naye akitua kutoka Manchester City mwaka 2021.