Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huu ndo ukweli wa ngoma ya Kasongo!

Muktasari:

  • Hiki ni kibwagizo cha wimbo maarufu wa zamani wa Kasongo, ambao kwa siku za hivi karibuni ndani na nje ya nchi umejipatia umaarufu mkubwa zaidi hasa katika mitandao ya kijamii na kitaani.

'KASONGO ye yeee, mobali na ngai...

Kasongo nga nawe ooh....

Zonga libala eeh...'

Hiki ni kibwagizo cha wimbo maarufu wa zamani wa Kasongo, ambao kwa siku za hivi karibuni ndani na nje ya nchi umejipatia umaarufu mkubwa zaidi hasa katika mitandao ya kijamii na kitaani.

Ni kibwagizo cha wimbo huo uliotungwa na kuimbwa na bendi ya Kikongo ya Super Mazembe, iliyokuwa na maskani yake jijini Nairobi.

Umaarufu wa kibwagizo hicho umetokana kuambatanishwa na video fupi inayomuonyesha mnyama ngiri na harakati zake porini dhidi ya wanyama jamii ya paka wakubwa.

Ni video zinazoonyesha uwezo wa mnyama huyo jamii ya nguruwe, alivyojaaliwa kasi na ujasiri wa kukabiliana na wanyama wakali kama chui, simba, mbwa mwitu, fisi na wengineo. Pia hutumiwa kwa vichekesho vingine tofauti na vya ngiri.

Hata hivyo, huenda ni watu wachache wanaojua kama kibwagizo hicho kinachosindikiza video hizo fupi ni moja ni mistari iliyomo katika wimbo uliowahi kutamba miaka ya 1980.

Wimbo huo huo uliimbwa na bendi hiyo ya Kikongo ya Super Mazembe, iliyoweka maskani yake kwa majirani zetu, Kenya ikitokea DR Congo (zamani Zaire) kuanzia mwaka 1974. Kabla ya kuingia Kenya na kufahamika kwa jina hilo, bendi hiyo ikiwa Kongo ilifahamika kama Super Vox na iliundwa na wanamuziki nguli waliotamba barani Afrika hususani ukanda wa Afrika Mashariki.

Kama ilivyo kwa asilimia kubwa ya nyimbo za zamani kusimulia mikasa ya kweli, ndivyo ilivyo kwa wimbo huo wa Kasongo uliotungwa na kuachiwa mwaka 1980, ukiwa na jina halisi la mmoja wa wanamuziki wa bendi hiyo aliyefahamika kama Kasongo wa Kanema.

Mwanamuziki huyo Mkongomani, aliyekuwa anamudu kupiga gitaa, kuimba na kutunga nyimbo alifariki dunia Aprili 14, 2020 na kuzikwa jijini Nairobi.

Mkongwe aliyeondoka duniani akiwa na umri wa miaka 73, aliwahi kufanya kazi pia na Super Virunga ya Samba Mapangala na alishiriki pia kuimbisha katika wimbo maarufu unaotamba kipindi hiki cha Krismasi uitwao 'Kakolele Viva Christmas' akiwa pamoja na Baba Gaston Ilunga wa Ilunga.

Kasongo alikumbwa na mauti alipokuwa nyumbani kwake eneo la Lang'ata, jijini Nairobi baada ya kuugua kwa muda mrefu tangu alipopata kiharusi na kuzikwa katika makaburi maarufu ya eneo hilo la Lang'ata, huku akiwa ameacha mke na watoto sita.


KISA CHA KASONGO

Kwa mujibu wa duru za kimuziki, wimbo huo wa Kasongo ni kisa cha kweli na ulitungwa kama utani kabla ya kuachiwa mwaka 1980 na wanamuziki wa Super Mazembe.

Inadaiwa kuwa, Kasongo wa Kanema, alitoweka ghafla katika kambi ya bendi hiyo kwa siku kadhaa, hivyo wanamuziki wenzake wakaona ni vyema wakamjulie hali nyumbani kwake eneo la Eastleigh, jijini Nairobi alipokuwa akiishi enzi hizo, ikizingatiwa zama hizo hakukuwa na simu janja, intaneti, wala mitandao ya kijamii ambavyo vingerahisisha mawasiliano baina yao.

Inaelezwa wanamuziki hao walipofika nyumbani kwa Kasongo aliyekuwa akiimba na kucharaza gitaa la rythm walikutana na kilio cha shemeji yao, yaani mke wa mwanamuziki mwenzao, aliyedai kuwa mumewe ana siku kibao hayupo hapo na kumpa wasiwasi sambamba na watoto wanaomuuliza kila mara baba yao.

Bibie huyo aliamua kumwaga mchele huo kwenye kuku wengi baada ya kuelezwa na mashemeji zake kwamba walifika nyumbani hapo kumtafuta, jambo lililomtia simanzi mkewe kwa kujua kwa vyovyote mashangingi ya jiji la Nairobi yatakuwa wamemnsa na kumpa hifadhi kwa siku zote ambazo hakuonekana.

Lakini kama mke, alijikaza na kuwaeleza wanamuziki wenza wa mumewe kwamba ana hofu na wasiwasi mkubwa huko alipo kama yupo salama na ikiwezekana wamjulishe arudi nyumbani, kwani hata watoto wanamuulizia baba yao.

Kama zilivyokuwa tabia za wanamuziki wengi wa zamani kutungia nyimbo matukio ya kweli yanayowazunguka, wanamuziki hao chapu kwa haraka wakapata wazo la kutunga wimbo huo wa Kasongo wakiwa bado wapo sebuleni mwa nyumba ya mwanamuziki wenzao, lengo likiwa ni kutaka kumfikishia ujumbe wa mkewe, popote alipokuwapo kwamba anapaswa kurejea kuitunza ndoa yake.

Na kama ambavyo mkewe alivyokuwa akiwalalamikia kwamba ana wasiwasi na usalama wa Kasongo huko aliko, ndivyo mistari ya wimbo huo unavyojieleza, kwani hawakuwa na njia nyingine ya kumfikishia ujumbe kwa vile simu za mkononi na mitandao haikuwapo enzi hizo.

Tafsiri ya maneno hayo ya Kilingala ya wimbo huo kuanzia hicho kibwagizo cha 'Kasongo ye yeee, mobali na ngai... Kasongo nga nawe ooh....Zonga libala eeh...' kwa kiswahili maana yake ni; 'Kasongo mume wangu, mie naatabika huku, tafadhali rudi nyumbani kwenye ndoa yako...'

Kifupi ni wimbo unaozungumzia kisa cha mkewe kumlilia Kasongo, huko alikokuwa amehifadhiwa, ajitokeze na kurejea nyumbani kuiendeleza ndoa yake, kwani yeye mkewe ana wasiwasi na hata watoto hawana amani kwa kutomuona Kasongo hapo nyumbani...!

Mara baada ya ngoma hiyo kutoka, huku Kasongo mwenyewe akishiriki kuuimba, ulikuja kujipatia umaarufu mkubwa na kuitangaza zaidi Super Mazembe iliyokuja kusambatika miaka mitano baada ya kuachiwa kwa Kasongo na kuzaliwa Bana Mazembe. Mbali na kibao hicho, Super Mazembe iliyowahi kufanya kazi Zambia na Tanzania kabla ya kuhamia Kenya, iliwahi kutamba na nyimbo nyingine kama Shauri Yako (ambao ulishinda tuzo ya BBC ya Wimbo Bora wa Karne), Na Bimaka Te, Samba, Bwana Nipe Pesa na vinginevyo.

Haishangazi sana kuona baada ya kupita karibu miaka 40 tangu wimbo hio ulipoachiwa na kutamba, kwa sasa umerudi katika umaarufu zaidi kwa mistari yake kutumiwa kama kibwagizo cha kuchekesha katika video zinazomuonyesha ngiri na harakati zake.

Mwanaspoti linataka kuwaonyesha watoto wa 2000, kwamba hii ngoma haikuwa ya mchezo mchezo kama wanavyoutumia katika video hizo fupi za vichekesho mbalimbali mtandaoni kwa kuweka mistari mizima na tafsiri yake kujua Kasongo ilikuwa ngoma ya maana miaka 1980.

Mistari ya ngoma hiyo ndio hiyo hapo chini;


Wimbo: Kasongo

Msanii: Super Mazembe


Kasongo ye yeee, mobali na ngai

(Kasongo eee, mume wangu)

Kasongo nga nawe ooh

(Kasongo mwenzio nataabika)

Songa libala ee

(Rudi kwenye ndoa) x2


Kasongo yo yoyoo, mobali na ngai

Kasongo nga nawe ooh

Songa libala eee


Kasongo ye yeee, mobali na ngai

(Kasongo eee, mume wangu)

Kasongo nga nawe ooh

(Kasongo mwenzio nataabika)

Songa libala ee

(Rudi kwenye ndoa) x2


Nga na ndako Kasongo

(Wakati upo nyumbani Kasongo)

Miso na nzela

(Tulitamba mtaani)

Soki okozonga dia ee

(Ikiwa unarudi nyumbani mpenzi)

'Yebisa nga yee eee

(Nifahamishe nijue)


Kasongo ye yeee, mobali na ngai

(Kasongo eee, mume wangu)

Kasongo nga nawe ooh

(Kasongo mwenzio nataabika)

Songa libala ee

(Rudi kwenye ndoa) x2


Kasongo yo yoyoo, mobali na ngai

Kasongo nga nawe ooh

Songa libala eee


Kasongo ye yeee, mobali na ngai

(Kasongo eee, mume wangu)

Kasongo nga nawe ooh

(Kasongo mwenzio nataabika)

Songa libala ee

(Rudi kwenye ndoa) x2


Nga na ndako Kasongo

(Wakati upo nyumbani Kasongo)

Miso na nzela

(Tulitamba mtaani)

Soki okozonga dia ee

(Ikiwa unarudi nyumbani mpenzi)

'Yebisa nga yee eee

(Nifahamishe nijue)


Kasongo ye yeee, mobali na ngai

(Kasongo eee, mume wangu)

Kasongo nga nawe ooh

(Kasongo mwenzio nataabika)

Songa libala ee x2


Libala na ndako Kasongo

(Hii ndio aina ya ndoa, Kasongo)

Batunaka ngai

(Wote wapo bize kuniuliza mimi)

Tata azali wapi eee

(Baba yuko wapi)

Naloba nini ee

(Niseme nini mimi)


Kasongo ye yeee, mobali na ngai

(Kasongo eee, mume wangu)

Kasongo nga nawe ooh

(Kasongo mwenzio nataabika)

Songa libala ee

(Rudi kwenye ndoa) x2


Kasongo ye yeee, mobali na ngai

(Kasongo eee, mume wangu)

Kasongo nga nawe ooh

(Kasongo mwenzio nataabika)

Songa libala ee