Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jux anaisubiri kwa hamu ndoa Nigeria

JUX Pict

Muktasari:

  • Februari 07 mwaka huu, Jux alifunga ndoa na mfanyabiashara na mwigizaji wa Nigeria, Priscilla iliyohudhuriwa na ndugu na marafiki wa karibu akiwemo Diamond Platnumz, Zuchu, S2kizzy, Ommy Dimpoz na wengineo.

BAADA ya kufunga ndoa Tanzania, Msanii wa Bongo Fleva, Juma Jux na mkewe Priscilla Ojo rasmi wametangaza ndoa nyingine ya kikabila itakayofungwa Aprili 17, Nigeria.

Februari 07 mwaka huu, Jux alifunga ndoa na mfanyabiashara na mwigizaji wa Nigeria, Priscilla iliyohudhuriwa na ndugu na marafiki wa karibu akiwemo Diamond Platnumz, Zuchu, S2kizzy, Ommy Dimpoz na wengineo.

Akizungumza na Hip TV ya Nigeria, Jux ambaye kwa sasa yupo nchini humo kwa maandalizi ya harusi hiyo, alisema ana shauku na harusi hiyo ya kitamaduni hasa kwenye mavazi na vyakula vya Nigeria.

"Nina furaha kubwa kuhusu harusi yangu ya kikabila inayokuja hivi karibuni. Siwezi kusubiri kuvaa Agbada. Nitawaleta wategemezi wangu wote kutoka Tanzania. Siwezi kusubiri kushuhudia utamaduni. Tayari napenda vyakula kama eba, pilau la jollof, bata mzinga, nk."

Aliongeza, harusi hiyo itahudhuriwa na watu mbalimbali kutoka Tanzania marafiki zake na ndugu wa karibu.

Hii inakuwa ndoa ya kwanza kwa msanii huyo anayetamba na kibao cha 'Si Mimi' akimuoa binti wa mwigizaji maarufu wa Nollywood, Iyabo Ojo.

Wawili hao walianza mahusiano Agosri 2024 huku penzi lao likishamiri na kuteka mitandao ya kijamii ya ndani na nje ya Tanzania kutokana na umaarufu wao.

Kabla ya Jux kuwa na mahusiano na Priscilla alikuwa na Karen Bujulu ambaye hakudumu nae muda mrefu wakaachana.