Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Khadija Kopa afichua posa ya Zuchu

Posa Pict

Muktasari:

  • Zuchu na Diamond inadaiwa ni wapenzi wa muda mrefu mbali na kufanya kazi ya muziki pamoja katika lebo ya WCB, huku kila mara wakidaiwa kutibuana na kurudiana.

MOJA ya stori kubwa mwezi huu ni ndoa ya Diamond Platnumz na Zuchu huku wengi wakijiuliza kama itakuwepo au ni drama tu kama walivyozoea kwa wasanii hao wa Bongo Fleva.

Nyota hao ambao anafanya vyema kwenye muziki ndani na nje ya nchi, wamekuwa wakifuatiliwa sana na mashabiki na wadau wa muziki kutokana na ukaribu hao na mara kadhaa wamekuwa wakihusisha na ndoa na kudaiwa mambo yanaenda vizuri na jambo litatimia.

Hata hivyo, kilichopo kwa sasa ni kuhusu posa ya Diamond na ilianza kama utani wengi wakijua ni kiki tu na msanii huyo anataka kutoa wimbo katika 'Valentine Day' iliyofanyika Ijumaa ya wiki iliyopita.

Kukawepo kwa habari posa hiyo ilipelekwa lakini ikakataliwa ndiyo maana hakukuwa na chochote, lakini mama mzazi wa Zuchu, Hadija Kopa amefunguka ukweli wa jambo hilo na ameliambia mwanaspoti lililofuatilia kwa undani na amesema habari hizo hazina ukweli wowote.

"Kwanza niwaambie watu mambo ya ndoa huwa mpangaji ni Mungu na kuhusu habari za wazazi tumekataa barua ya posa siyo za ukweli, sisi hatujaona barua yoyote kutoka kwa Diamond, zaidi ya kusikia tu huko mitandaoni," alisema Khadija Kopa na kuongeza;

"Halafu watu wanataka waelewe hili, furaha ya Zuchu ndiyo furaha yangu na familia yake, sasa sisi tukatae posa kwa ajili ya nini? Maana hadi mipango ya posa hiyo inapangwa ni lazima mwanamke husika ajue, sasa kama wamekubalina watoto, kwa nini wazazi wapinge?

"Tena sio tu barua ya posa kwa Diamond, sisi tunapokea barua ya mtu yeyote atakayehitaji kumposa Zuchu, kwa nini waseme Diamond tu? Kikubwa Zuhura (Zuchu) akikubali sisi hatuna pingamizi, ndoa ni heshima bana na ni jambo la kheri. Hivyo achana na wapiga midomo ya mitandaoni hao waongea tu."

Mwimbaji huyo nyota wa muziki wa taarabu amesema katika mambo anayopenda, ni kutoingilia mambo ya Zuchu pindi anapoandika vitu vya kuachana mitandaoni zaidi ya kumjenga kuwa na uvumilivu katika maisha.

"Naviona vitu anavyoandika Zuchu, sasa mie siwezi kumuingilia...mambo ya kitoto hayo, ila kama mzazi huwa nampa somo la uvumilivu katika maisha ndiyo nguzo kubwa kwake," amesema Khadija wa kundi la TOT Taarabu.

Zuchu na Diamond inadaiwa ni wapenzi wa muda mrefu mbali na kufanya kazi ya muziki pamoja katika lebo ya WCB, huku kila mara wakidaiwa kutibuana na kurudiana na juzi kati Siku ya Valentine, Mondi aliandika ujumbe mzito wa mahaba kwa mpenziwe huyo kuonyesha wapo sana pamoja.