Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kobisi wa Kombolela tofauti na uhalisia

KOBISI Pict

Muktasari:

  • Kobisi alianza kazi ya sanaa mwaka 2000 akiwa na kundi la sanaa la Mwananyamala Arts akiwa kama mwongozaji wa wasanii.

MSANII mkongwe wa Bongo Movie, Lumole Matovolwa 'Kobisi' amesema anayoyaigiza kwenye tamthilia ya Kombolela hayahusiana na maisha yake binafsi.

Kobisi alianza kazi ya sanaa mwaka 2000 akiwa na kundi la sanaa la Mwananyamala Arts akiwa kama mwongozaji wa wasanii.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kobisi alisema anachokifanya kwenye tamthilia hiyo pendwa nchini kwa sasa ni kile alichoelekezwa na mwongozaji na ni tofauti na maisha yake halisi.

Aliongeza anaishi maisha ya uswahilini hivyo huenda alichokiigiza ni miongoni mwa vitu anavyoviona kila kukicha.

"Mimi ni mcheshi, lakini siyo mzembe kama Kobisi, maisha yake sifananii hata kidogo, ile ni kazi na msanii kazi yake ni kufuata muongozo ulivyo," anasema na kuongeza

"Kuna mama nilikutana naye aliniambia anavyoniona kwenye maigizo ni tofauti na anavyoniona kwenye uhalisia. Maigizo yatabaki kuwa maigizo, ndiyo maana leo waigizaji wengi wanasema wao ni mastaa wanaigiza maisha, mimi napanda daladala lakini kuna waigizaji hawawezi."

Mbali na kuigiza pia Kobisi alikuwa 'Video King' kwenye wimbo wa Bahati Bukuku 'Kampeni' uliotoka miaka 10 iliyopita.