Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lupita Nyong’o: Mrembo Mkenya anayetetemesha Hollywood

Lupita Nyong’o, mrembo wa Kikenya

Muktasari:

Warembo hao waigizaji wanatengeneza majina yao hapo na kuwa mashuhuri, wanapata umaarufu na hatimaye wanavuna pesa za maana kutokana na ushiriki wao kwenye sinema hizo.

HOLLYWOOD ni maskani ya wanawake warembo na wenye vipaji. Kiwanda namba moja cha filamu duniani, ambapo wanawake na mabinti wazuri waigizaji wamekuwa wakiibukia kila kukicha.

Warembo hao waigizaji wanatengeneza majina yao hapo na kuwa mashuhuri, wanapata umaarufu na hatimaye wanavuna pesa za maana kutokana na ushiriki wao kwenye sinema hizo.

Baadhi ya waigizaji mahiri kama Angelina Jolie wamekuwa wakipiga mamilioni ya pesa. Kwenye kiwanda hicho, kwa sasa kuna jina jipya limeibuka kwa kasi na kutishia mengine yaliyotangulia. Lupita Nyong’o, mrembo wa Kikenya. Anatikisa Hollywood.

Akiwa hata hana muda mrefu Hollywood, mrembo huyo tayari ameshaingia kwenye orodha ya mabinti wanaopiga pesa za maana kwenye kiwanda hicho cha sinema. Lupita anatajwa kuwa na kipato kinachofikia Dola 10 milioni.

Kwa mujibu wa CelebrityNetWorth.com, tovuti inayojihusisha na utajiri wa pesa za wasanii, unamtaja mrembo huyo raia wa Kenya kuwa mmoja wa waigizaji wenye nafasi kubwa ya kupiga pesa za maana kutokana na mwonekano wake na umahiri kwenye filamu na tasnia ya mitindo, wakati starsmeasurements.com iliyofanya mahojiano na mrembo huyo imefichua utajiri wake kuwa ni Dola 10 milioni.

Jinsi anavyopiga pesa

Lupita ni kipaji kipya kwenye tasnia ya filamu na mitindo. Jina lake limeanza kuwa kubwa Hollywood baada ya kushirki kwenye filamu ya ‘12 Years A Slave’, ambapo Jumapili iliyopita alifanikiwa kushinda Tuzo ya Oscar akiwa Mwigizaji Bora Msaidizi kwenye sinema hiyo.

Kitendo cha kuibuka mshindi kimemfanya Lupita kupiga pesa ya maana baada ya kuvuna Dola 500,000. Lakini, huo ni mwanzo na Lupita ataendelea kuvuna pesa zaidi kutokana na sasa kuvutia kampuni nyingi ambazo zitahitaji kufanya naye biashara kama balozi wao. Lupita pia ni mwanamitindo na mara kadhaa amekuwa akipiga pesa kwa kuonyesha mitindo ya mavazi.

Lupita alipiga pesa pia kwa kushiriki kwenye filamu za ‘The Constant Gardener’, ‘The Namesake’, ‘East River’, ‘Uncle Vanya’, ‘The Winter’s Tale’ na kwenye video ya wimbo ‘The Little Things You Do’ ya mwimbaji, Wahu.

Filamu yake ya kwanza kwenye uigizaji wenye malengo ilikuwa ya ‘East River’ na kisha akapata dili la kucheza kwenye ‘12 Years A Slave’, ambapo aliigiza kama Patsey. Lupita ana dili nyingi tu za pesa, ikiwamo kupamba majarida ya mitindo likiwamo Jarida la Dazed & Confused la Uingereza.

Lupita ni nani?

Lupita ni binti wa Kikenya. Mwigizaji na mwongozaji wa video ambaye kwa sasa anatumia sanaa hiyo kujitafutia utajiri. Lupita alizaliwa Machi 1, 1983 huko Mexico City, Mexico, mahali ambako baba yake alikuwa Profesa kwenye Chuo Kikuu cha El Colegio de Mexico.

Alikulia jijini Nairobi, Kenya, kabla ya kwenda kusoma Mexico, akijifunza Kihispaniola. Lupita aliendelea na masomo na kuhitimu kwenye Chuo cha Hampshire alikopata Shahada ya Masuala ya Filamu na Sanaa za Maonyesho.

Baada ya kuhitimu aliingia kwenye tasnia ya filamu na kushiriki sinema kadhaa na kufanikiwa kutwaa Tuzo ya Herschel Williams mwaka 2011. Lupita ni jina lenye asili ya Mexico, pia ni mtoto wa pili kuzaliwa kwenye familia ya watoto sita.

Lupita kwa sasa anaishi Brooklyn, Marekani na ana uwezo wa kuzungumza lugha nne kwa ufasaha, nazo ni Kiswahili, Kiingereza, Kihispaniola na Kijaluo.

Familia

Wazazi wake walikuwa wakimbizi wa kisiasa nchini Mexico. Wazazi hao waliondoka Kenya wakati huo mama yake Lupita akiwa na ujauzito uliomzaa Lupita.

Wazazi wa Lupita wana heshima kubwa Kenya kutokana na wote walikuwa na elimu ya kutosha na kujihusisha kwenye mambo ya kisiasa.

Peter Anyang Nyong’o alianza siasa mwaka 1992 baada ya kufanya kazi akiwa Profesa. Alikuwa akifundisha nchini Kenya, lakini alifundisha pia vyuo vikuu kadhaa vya Mexico. Baadaye Peter alirudi Kenya na kujiingiza jumla kwenye siasa na kuwa Seneta kwenye Bunge la Kenya.