Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mavazi ya kike yalivyotibua ndoa ya Dullivan

DULLIVAN Pict

Muktasari:

  • Dullivan ameongeza kusema alijaribu kueleza mavazi hayo ni sehemu ya kazi yake ya kuigiza na kuelimisha pamoja na kuburudisha jamii, lakini maelezo hayo hayakubadilisha msimamo wa wazazi wa mpenzi wake.

MSHEKESHAJI maarufu mitandaoni, Dullivan amefichua mavazi ya kike anayovaa wakati wa kutengeneza maudhui ya uchekeshaji ndiyo yaliyosababisha kuvunjika kwa uhusiano wake na aliyekuwa mpenzi wake, Mimimalu.

Akizungumza na Mwanaspoti hivi karibuni, Dullivan alisema alikuwa katika hatua za mwisho za kufunga ndoa na mpenzi wake huyo kabla ya kukumbana na pingamizi kutoka kwa wazazi wa binti huyo.

Amesema wazazi wa Mimimalu hawakuwa tayari kumuunga mkono kutokana na taswira anayoionyesha kwenye kazi yake ya sanaa, hasa pale anapoonekana amevaa mavazi ya kike katika baadhi ya kazi zake za uchekeshaji.

DULL 01

Kwa mujibu wa Dullivan, jitihada mbalimbali zilifanyika kueleza mavazi hayo ni sehemu ya kazi na hayawakilishi maisha yake halisi, lakini wazazi hao hawakubadili msimamo wao.

Hali hiyo ilizidi kuleta sintofahamu katika uhusiano wao na hatimaye ndoto yao ya kufunga ndoa ikafikia mwisho kabla ya kutimia.

“Nilikuwa na mwanamke wangu na tulikuwa tumepanga kuoana, lakini wazazi wake walinikataa kwa sababu ya mavazi ya kike ninayovaa kwenye kazi yangu ya uchekeshaji. Mwishowe tukashindwa kuendelea na mahusiano,” amesema Dullivan.

Dullivan ameongeza kusema alijaribu kueleza mavazi hayo ni sehemu ya kazi yake ya kuigiza na kuelimisha pamoja na kuburudisha jamii, lakini maelezo hayo hayakubadilisha msimamo wa wazazi wa mpenzi wake.

DULL 02

"Kutokana na hali hiyo, uhusiano wetu uliendelea kukumbwa na changamoto zilizokuwa zikiongezeka kadri siku zilivyokuwa zinasonga mbele, hali iliyosababisha mimi na mwenzangu kushindwa kutimiza ndoto yetu ya kuingia kwenye ndoa."