Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mazito harusi ya mchekeshaji Eliud

ELIUD Pict


MSANII wa vichekesho, Eliud Samwel amefunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi, Beatrice Lucas, lakini nyuma ya pazia wakafanya mambo mazito katika ukumbi wa Lamata Village jijini Dar es Salaam katika sherehe iliyopambwa na burudani mbalimbali huku ikihudhuriwa na mastaa mbalimbali wakiwamo wale wa vichekesho.


Wasanii waliohudhuria katika sherehe hizo walijaribu kumchekesha bwana harusi pamoja na mkewe kwa staili tofauti  zikiambatana na zawadi walizokuwa wameziandaa.


Kundi la vichekesho la Watu Baki lilitoa kali ya mwaka katika sherehe hiyo baada ya kutoa zawadi ya tenga lililojaa nyanya, parachichi, tambi, vitunguu, pilipili, mboga za majani na mazao mengine tofauti pamoja na na tisheti mbili - moja ikiwa ya mchekeshaji huyo na nyingine ya mkewae pamoja na picha kubwa ya Eliud ya utotoni ambayo iliwekwa kwenye fremu.

ELIU
ELIU

Nao wasanii wa Jua Kali waliopo chini ya Lamata Village wakiongozwa na Lamata Mwendamseke waliingia ukumbini wakiwa wamevaa sare ya nguo yenye rangi ya njano, ambapo wanaume walivaa suti kama ile ya Eliud ambayo hupenda kuitumia wakati akiwa kwenye vichekesho vyake huku wanawake wakivaa magauni ya njano.

Tukio hilo lilikuwa kama 'saprazi' kwa Eliud aliyeshindwa kuvumilia akaomba 'maiki' kwa mshehereshaji wa sherehe hiyo ili azungume kwa dakika moja ambapo alianza kusema maneno haya: "Kwa kweli hii ni saprazi kwangu. Yaani mmeamua kuvaa nguo yangu ya ofisi? Na najua huwa hamuipendi rangi ya njano, lakini sasa mtafanyaje ndiyo hivyo mkajikusanya mkapanga mvae ilimradi tu mfanane na nguo yangu ya kazini."

ELIU 02

Eliud mwenyewe muda wote wa shughuli hiyo kanisani na hata kwenye ukumbi watu waliohudhuria walionekana kufurahi na mara kadhaa alifanya vituko vya hapa na pale katika kukoleza furaha iliyokuwapo.

Picha lilianza kwa Eliud akiwa kanisani kuwaringishia pete wageni baada ya kupokea cheti cha ndoa, ambapo alikinyanyua mkononi na kuonyesha pande zote walipokuwa wamekaa watu na lilipofika tukio la kukata keki ilikatwa kwa kutumia panga.

Utamu zaidi ulikuwa wakati wa kulishana keki, ambapo mke wa Eliud alimlisha kwa mdomo mumewe kitendo ambacho bwana harusi aliona aibu ambapo aliamua kuficha uso na ni hapo vicheko ukumbini vilitawala.

Kwenye suala la utambulisho, mchekeshaji huyo alimuita mkewe sukari huku akisema atamuita Bite na siyo Beatrice kama wanavyomuita wazazi wake na hapo akampokonya kifeni ambacho mkewe alikuwa anajipulizia na kuanza kujipulizia yeye.

ELIU 03
ELIU 03

"Mke wangu anaitwa Beatrice ila mimi humuita sukari hapa, wakati mwingine namuita Bite maana neno la Beatrice ni refu sana kulitamka," alisema Eliud. Yote kwa yote Mwanaspoti lilipopiga stori na Eliud kumpa pongezi na kuzugumza machache juu ya harusi hiyo, alishukuru, kisha akamwaguka:

"Nashukuru sana kwa pongezi zako Mungu ni mwema. Hili limemalizika salama kilichobakia ni kutafuta watoto sasa (kicheko).

Kiukweli nawashukuru sana watu wote waliohudhuria kwenye harusi yangu na wafanyakazi wenzangu wa Lamata Village kwa saprazi ya suti yangu ya rangi ya njano, kumbe walikuwa wanaona nafaidi navyoivaa na wao wakaona waivae. Pia timu nzima ya Cheka Tu ikiongozwa na Coy Mzungu wamenipa ushirikiano mkubwa sana pamoja na Watu Baki."