Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndevu zinaongeza mvuto kwa wanawake? Mwanamume fanya hivi

NDEVU Pict

Muktasari:

  • Ndevu siyo tu fasheni, ni mvuto kimwonekana na kuna wanawake wanavutiwa wakiona waume zao wana ndevu na huenda mbali zaidi na kuiwasaidia kuwashauri namna ya kuziweka ili zizidi kuwavutia.

MOJA ya vitu vinavyompa mwanamume mwonekano mzuri usoni ni ndevu. Mwanamume anaonekana wa kisasa pale anapojua namna ya kuzitengeneza zivutie.

Ndevu siyo tu fasheni, ni mvuto kimwonekana na kuna wanawake wanavutiwa wakiona waume zao wana ndevu na huenda mbali zaidi na kuiwasaidia kuwashauri namna ya kuziweka ili zizidi kuwavutia.

Hata hivyo, wapo ambao hawana na wanatamani kuwa nazo na wengine wanazo lakini wanashindwa namna ya kuzihudumia. Wengi hupuuza na hivyo kuwa na mwonekano mbaya.

Je, ndevu zinaongeza mvuto kweli? Kama ndiyo, mwanamume anatakiwa afanye nini ili kuzifanya zivutie kwake na kwa wanaomtazama? Ili uonekane unavutia, zingatia mambo haya wewe mwenye ndevu.

NDEV 01

USAFI, MATUNZO YA NGOZI

Mbali na lishe ambazo wataalamu wanashauri kwa ajili ya ukuaji wa ndevu, lakini usafi wa ngozi ya uso ni muhimu ili kuzipa afya na kuosha mara kwa mara uso kwa sabuni maalumu, husaidia kuzibua na kuondoa uchafu na mafuta yasiyohitajika, hivyo, kuzifanya zikue.

Pia kwa kutumia mafuta maalumu ya ndevu husaidia kulainisha ngozi na kufanya ziwe laini na zenye kung’aa.

NDEV 06

UVUMILIVU NI MUHIMU

Wengi hukata tamaa mapema wanapoona ndevu hazikui kwa kasi wanayotaka. Ukweli ni kwamba ukuaji wa ndevu hutofautiana kati ya mtu na mtu, kutegemea na vinasaba pamoja na homoni za mwili.

Hivyo, hakuna njia ya mkato ni suala la subira, mwendelezo wa kujitunza na kujiamini. Wale wanaovumilia mara nyingi ndiyo hufikia matokeo bora zaidi.

NDEV 02

NDEVU NA SURA

Kwa wanaotaka kuongeza mvuto kupitia ndevu, wataalamu wanashauri mambo kadhaa ya msingi. Kwanza, chagua mtindo wa ndevu unaoendana na umbo la uso wako badala ya kuiga kila unachoona mitandaoni. Pili, epuka kuziacha ndevu zikue bila mpangilio, punguza na zipange mara kwa mara ili ziwe na mwonekano nadhifu.


CHANGAMOTO ZA NDEVU

Mbali na faida zake, ndevu pia zina changamoto ambazo wanaume wengi hukutana nazo. Baadhi hupata muwasho wa ngozi, chunusi chini ya ndevu au ukuaji usio sawa.

Hii inaonyesha, kuwa na ndevu nzuri si suala la kuziacha zikue tu, bali kunahitaji matunzo maalum na uangalizi wa karibu ili kuepuka matatizo hayo.

NDEV 03

MAKOSA WANAYOFANYA WANAUME

Wanaume wengi hupunguza mvuto wa ndevu zao bila kujua kwa kufanya makosa kama kutopangilia ndevu mara kwa mara, kutumia bidhaa zisizo sahihi au kuziacha zikue bila usafi.

Wengine huamini kunyoa mara kwa mara kunachochea ukuaji wa ndevu, jambo ambalo si sahihi kitaalamu. Kuepuka makosa haya kunaweza kusaidia ndevu kuwa nadhifu na kuvutia zaidi.


JE, NDEVU ZINAONGEZA MVUTO?

Pamoja yote, bado mjadala kuhusu mvuto wa ndevu unaendelea kushika kasi katika jamii. Wapo wanaoamini huongeza mvuto na wengine wakiona ni chaguo binafsi lisilo na ulazima mkubwa katika mwonekano wa mwanamume.

NDEV 04

MAONI YA WADAU

Mke wa msanii wa Hip Hop nchini, Afande Sele,Imani Makongoro anaona ndevu kama sehemu ya hadhi ya mwanamume.

“Ndevu zinampa mwanamume mwonekano mzuri na zinaongeza mvuto, kuna muda unatamani tu kumshika, lakini kama hana nahisi kama hajakamilika vizuri."

Pelagia Daniel anasema; “Kwa upande wangu, mwanamume mwenye ndevu safi na zilizopangiliwa vizuri anaonekana kuvutia zaidi. Inaonyesha anajitambua na anajali mwonekano wake.”

Kwa upande mwingine, Olipa Assa ana mtazamo tofauti kuhusu suala hilo.

"Kwangu kikubwa zaidi kwa mwanamume ni akili ya kutafsiri vitu kwa uharaka, kuamua kwa hekima, hivyo mvuto kwa upande wangu ni utashi alionao, haijalishi anamwonekano gani kwa kipindi hicho, mwonekano unatengenezwa.

“Mimi naamini mvuto wa mwanamume hautokani na ndevu pekee. Kuna watu hawana ndevu lakini wanavutia sana. Kikubwa ni usafi na kujiamini."

NDEV 05

USHAURI WA ANTI

Kipenzi, ndevu zinaweza kuwa nyenzo muhimu ya kuongeza mvuto wa mwanamume ikiwa zitatunzwa ipasavyo. Hata hivyo, hazipaswi kuwa kipimo pekee cha mvuto, kwani kuna mambo mengine kama usafi wa mwili, mavazi na kujiamini yana mchango mkubwa zaidi.

Mwishowe, mwanamume anapaswa kuelewa mvuto wa kweli haupo tu kwenye ndevu, bali katika namna anavyojiweka, anavyojitunza na anavyojiamini. Ndevu ni nyongeza tu lakini ikitumika vizuri, inaweza kubadilisha kabisa taswira ya mwanamume mbele ya jamii.

Wewe mwanaume, usitumie mwonekano wako mzuri unaochangiwa na ndevu kuwa kikwazo cha namna yoyote iwe kwa wenzako au wanawake. Kama mwanamume atajitunza vizuri kiakili na kimaisha anamvutia mtu yoyote bila ndevu.