Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Noma yamkalia kooni Kombolela? Watayarishaji wafunguka baada ya ‘vita’ ya mashabiki

KOMBELELA Pict

USHINDANI mkali kati ya tamthilia za Noma na Kombolela zinazorushwa kupitia Chaneli ya Sinema Zetu katika kisimbuzi cha Azam TV, umeendelea kuteka mijadala kwenye mitandao ya kijamii na mtaani, huku mashabiki wakigawanyika kuhusu ipi inastahili kushika namba moja.

Kombolela inayoruka kwa nusu saa kila siku za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kuanzia saa 1:30, inatayarishwa na Abdul Usanga, ambapo ilizinduliwa rasmi Desemba 3, 2024 na tangu hapo imekuwa ikifanya vizuri kwa kujijengea mashabiki wa kudumu.

Kwa upande mwingine, Noma ya Adam Kibaro, ilianza kuonyeshwa Septemba 5, 2025 ikiruka paia siku hizo kwa muda wa nusu saa kuanzia saa 1:00 usiku, ndani ya muda mfupi imekuja juu kwa kasi kubwa, ikianza kutikisa nafasi ya Kombolela.

Katika mahojiano na Mwanaspoti, watayarishaji hao wamefunguka kuhusu ushindani huo unaoendelea mitandaoni, huku kila mmoja akionesha kujiamini na kazi yake.

KOMBO 03

Adam Kibaro amesema:

“Tunachokiona mitandaoni ni ishara nzuri kwamba watu wanafuatilia kazi zetu kwa karibu sana, Noma haikuja kushindana kwa maneno, imekuja kuonesha ubora wa hadithi, ubunifu na uhalisia wa maisha ya kila siku.

KOMBO 04

"Kama watu wanaona inaizidi Kombolela, hiyo ni tafsiri yao kutokana na wanachokipata. Sisi tunaendelea kuboresha kila sehemu, kuanzia uigizaji hadi namna ya kuwasilisha simulizi, ili watazamaji wetu waendelee kupata kitu kipya kila wakati.”

KOMBO 01

Kwa upande wake, Abdul Usanga ameeleza:

“Kwanza kabisa tunaheshimu kazi ya wenzetu wa Noma, lakini ukweli ni kwamba Kombolela imejijenga kwa muda na ina msingi imara kwa watazamaji. Haya yanayoendelea mitandaoni ni kawaida kwenye kazi zinazopendwa, mashabiki wetu wanajua nini wanakipata, ubora, uhalisia na muendelezo wa hadithi, hatuingii kwenye mashindano ya maneno, tunaacha kazi izungumze yenyewe.”

Licha ya maneno hayo ya kiungwana, mitandaoni hali ni tofauti. Wapo wanaosema Noma imekuja na kasi na mbinu mpya za usimulizi zinazovutia kizazi cha sasa, huku wengine wakisisitiza kuwa Kombolela bado ina uzito wa kipekee usiofikiwa kirahisi.

KOMBO 02

Ukweli unabaki kuwa, tamthilia hizi mbili zimefanikiwa kushika soko na kuibua ushindani unaochochea ubunifu zaidi katika tasnia ya filamu nchini.

Kwa sasa, macho ya wengi yako kwa watayarishaji hawa wawili kuona nani ataendelea kushika kasi, ni Noma au Kombolela?