Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Staili mpya nywele za Diamond zinatukumbusha 'Zilipendwa'

DIAMOND Pict

Muktasari:

  • Kwa mashabiki wake, mawimbi haya ni kivutio cha kisasa na ni moja ya mitindo ambayo wanataka kuiga. Kwa vijana wengi, mtindo huu unaonyesha jinsi gani wanamuziki wanavyoweza kuathiri maisha ya kila siku, na ndiyo maana wapenzi wa Diamond wanajikuta wakitafuta njia za kuiga staili hii katika maisha yao ya kila siku.

DIAMOND Platnumz ameendelea kuvuma kwa mtindo wake wa kipekee, akiwa na mabadiliko makubwa ya nywele ambayo yanaonekana kuwa kivutio kwa mashabiki.

Staili hizi mpya za nywele alizozionyesha kwenye wimbo wake mpya "Happy", zimeleta mabadiliko katika tasnia ya mitindo na muziki, huku mashabiki wake wengi wakitarajiwa kuiga kama ilivyokuwa kwenye wimbo wake maarufu "Zilipendwa" alioutoa mwaka 2017 akishirikiana na wasanii Mbosso, Harmonize, Rayvany, Lavalava na Queen Darleen ambao kwasasa hawapo lebo yake ya Wasafi.

Katika video ya "Zilipendwa", Diamond Platnumz aliwashirikisha wasanii hao waliokuwa wamevaa mavazi ya zamani kama suruali, nywele, na hii ilisababisha watu wengi kuiga mitindo hiyo.

Video hiyo ilikuwa na mvuto mkubwa, mashabiki walijikuta wakitafuta mavazi kama yale waliyoyaona kwenye video. Hivyo, staili za nywele ambazo Diamond ameonesha hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na mawimbi, rolaz, na wingi wa nywele za asili, zinatarajiwa kuwa maarufu miongoni mwa vijana na mashabiki wa muziki wake.

Hii ni ishara ya nguvu ya ushawishi wa Diamond Platnumz, ambaye ameendelea kuwa kipenzi cha vijana na kielelezo cha kuigwa katika mitindo na muziki, kama ilivyokuwa "Zilipendwa".

Wimbo huu mpya na staili zake za nywele zitakuwa sehemu muhimu ya mabadiliko makubwa kwenye jamii, na baadhi ya mashabiki wake wanajiandaa kuiga kila kitu anachofanya.

DIA 03

ROLAZ ZA KUSETIA WANAWAKE
Moja ya staili inayovuma na kutumiwa na wanawake wakati wa kuweka dawa ya nywele kichwani kama Relax, Kali na Wave. Sasa kutoka kwa Diamond Platnumz katumia hizo rolaz staili ya kunogesha video yake ya Happy, ambayo ni mtindo maarufu wa wanawake kutunza nywele zao.

Ingawa ni mtindo ambao mara nyingi umeonekana kwa wanawake, Diamond ameonesha kwa ujasiri jinsi mwanaume anavyoweza kuutumia na kuwa na mvuto wa kipekee. 

Katika video ya wimbo wake "Happy", Diamond ameonekana akitumia rolaz hizi, na staili hii imekuwa kivutio kwa vijana wanaoiga kila anachofanya na pia kwani unaleta muonekano wa kisasa na pia unahusisha utunzaji wa nywele. Hii ni sehemu ya ubunifu wa Diamond ambao unaendelea kuwa na ushawishi mkubwa kwenye mitindo ya vijana.

DIA 02

NYWELE NYINGI KICHWANI
Katika hatua nyingine ya mtindo wa nywele, Diamond ameonekana akitumia wingi wa nywele za asili, hii ni sehemu ya mabadiliko ya mitindo ambayo wengi wamekuwa wakivutiwa nayo. Wingi huu unahusisha nywele za kiasili ambazo hutumika kuleta muonekano wa kifahari na wa asili.

Diamond ameonekana katika video ya "Happy" akiwa na wingi huu wa nywele, na mashabiki wake wengi, hasa wanawake wameanza kuiga mitindo hii kwa kujivunia nywele zao za asili, hii inaendelea kuwa kivutio cha mitindo, ambapo wapenzi wa muziki wa Diamond wanachukua hatua ya kutunza nywele zao kwa njia ya asili, kuepuka matumizi ya kemikali na bandia.

DIA 01


NYWELE ZA MAWIMBI NA KOFIA
Pamoja na rolaz na wingi wa nywele za asili, Diamond ameonesha pia mtindo mwingine wa kuvaa nywele zenye mawimbi kwenye wimbo wake mpya "Happy". Mawimbi haya ni moja ya mitindo inayorudi kwa kasi na kuwa maarufu, na Diamond ameonesha jinsi mtindo huu unavyoweza kuleta mvuto na urembo wa kipekee.

Kwa mashabiki wake, mawimbi haya ni kivutio cha kisasa na ni moja ya mitindo ambayo wanataka kuiga. Kwa vijana wengi, mtindo huu unaonyesha jinsi gani wanamuziki wanavyoweza kuathiri maisha ya kila siku, na ndiyo maana wapenzi wa Diamond wanajikuta wakitafuta njia za kuiga staili hii katika maisha yao ya kila siku.