Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Siri nyuma ya majina ya mastaa wa filamu, tamthilia Bongo

MASTAA Pict


KATIKA ulimwengu wa sanaa, ikiwemo muziki na filamu, mashabiki wamezoea kuwaita mastaa fulani kwa majina wanayotumia katika kazi zao, ambapo majina hayo yamekuwa maarufu na yale halisi waliyopewa na wazazi wao yakisahaulika kabisa.


Mwanaspoti linakuletea baadhi ya mastaa ambao majina wanayotumia katika kazi zao za filamu au muziki yamekuwa maarufu na yale halisi waliyopewa na wazazi wao yakisahaulika kabisa.

MASTA 02

Mbosso (Bongofleva)

Jina la Mbosso lilianza kwenye muziki akiwa kwenye kundi la Yamoto Band, ambapo wakati huo alikuwa akitumia jina la kisanii “Maromboso.”

Baada ya kundi hilo kuvunjika na kuanza muziki wa solo, jina lake “Maromboso” lilibadilishwa na kufupishwa kuwa “Mbosso.” Hilo lilifanyika kama sehemu ya kuboresha brand yake ya muziki na kuifanya iwe rahisi kukumbukwa na mashabiki.

Baadaye aliongeza pia jina la heshima “Khan”, ambalo hutumika kama sehemu ya utambulisho wake wa kisanii (Mbosso Khan), likiwa na maana ya kuongeza hadhi na upekee kwenye muziki wake. Lakini jina lake halisi ni Mbwana Yusuf Kilungi.

MASTA 06

Bi Star (filamu, tamthilia)

Bi Star, ambaye jina lake halisi ni Shamila Rashid Ndwangila, ni mmoja wa wasanii wakongwe na mashuhuri wa filamu na tamthilia nchini Tanzania. Jina la Bi Star limekuwa likitambulika zaidi kuliko jina lake hilo halisi. Tamthilia aliyocheza ya Fukuto ndiko lilipatikana jina hilo baada ya msanii mwenzake Muhogo Mchungu kumpa jina hilo.

MASTA 03

Harmonize (Bongofleva)

Jina la Harmonize mwenyewe aliwahi kusema limetokana na neno la Kiingereza “harmony”, likimaanisha mpangilio mzuri wa sauti, jambo linaloakisi uwezo wake wa kuimba kwa utulivu na kuendana na midundo tofauti ya muziki. Harmonize limezoeleka sana kwa mashabiki wa muziki kuliko jina lake halisi Rajabu Kahali.

MASTA 04

Johari (filamu)

Johari lilikuwa maarufu baada ya kucheza filamu iliyokwenda kwa jina la Johari ambayo ndiyo ilimfanya ajulikane ndani na nje ya nchi ya Tanzania. Jina lake halisi ni Blandina Chagula.

MASTA 01

Diamond Platnumz (Bongofleva)

Diamond Platnumz, ambaye jina lake halisi ni Nasibu Abdul Juma, aliwahi kusema kuwa jina hilo limetokana na thamani kubwa kama almasi, na “Platnumz” likiongeza hadhi ya ubora, akilitumia kujijengea taswira ya msanii wa kiwango cha juu tangu alipoanza muziki.

MASTA 07

Muhogo Mchungu (filamu, tamthilia)

Kwa mujibu wake, jina la “Muhogo Mchungu” linatokana na historia yake ya kuuza mihogo, hasa aina yenye ladha chungu, kabla ya kuingia kwenye fani ya uigizaji. Jina hili linaashiria uthubutu wake na kupambana na maisha kupitia biashara hiyo.

Alisema kuwa alikuwa akivunja na kuuza mihogo michungu kama biashara yake kuu, hivyo jina hili linawakilisha maisha yake ya awali ya kutafuta kipato kabla ya kujulikana kama mwigizaji. Jina lake halisi ni Abdallah Mkumbillah, na amecheza tamthilia nyingi sana akianzia kwenye tamthilia ya Hujafa Hujaumbika, lakini alipata umaarufu kwenye tamthilia ya Fukuto akicheza baba wa watoto wawili, Nyamayao na Kibakuli, pamoja na nyumba ndogo Bi Star.

MASTA 05

Gabo (filamu, tamthilia)

Jina halisi la msanii huyu ni Salim Ahmed, lakini jina la kisanii anajulikana kama Gabo Zigamba.

Msanii huyo aliwahi kusema chimbuko la jina la Gabo ni “Gabon”, likiwa na maana ya “sauti isiyosikika”, na Zigamba ni ng’ombe wa kimila aliyekuwa akihusudiwa na Wasukuma zama za kale.