Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Oriana, mkewe Dybala anayepiga kotekote

Muktasari:

  • Dybala anayekipiga kama mshambuliaji au kiungo mshambuliaji pale Roma inayoshiriki Ligi Kuu Italia (Serie A), kwa sasa anauguza majeraha ya misuli ya paja na anatarajiwa kurejea uwanjani Desemba 2025.

Mashabiki wa AS Roma wana kiu ya kumuona Paulo Dybala 32, akirejea tena uwanjani, lakini upande wa pili staa huyo kiu yake ni kumuona mtoto wake wa kwanza na mkewe Oriana Sabatini, 29, ambaye ni mjamzito.

Dybala anayekipiga kama mshambuliaji au kiungo mshambuliaji pale Roma inayoshiriki Ligi Kuu Italia (Serie A), kwa sasa anauguza majeraha ya misuli ya paja na anatarajiwa kurejea uwanjani Desemba 2025.

Licha ya changamoto hiyo, mshindi huyo wa Kombe la Dunia akiwa na timu yake ya taifa ya Argentina, bado ana tumaini la kuendelea kufanya vizuri hasa kutokana na msukumo anaoupata kutoka katika ndoa yake.

Tangu mwaka 2018, Dybala amekuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Oriana, kufikia Julai 20, 2024, ndipo wakafunga ndoa katika jiji la nyumbani kwao la Buenos Aires nchini Argentina.

oriana 5

Mnamo Septemba 30, 2025, wanandoa hao wakatangaza kuwa wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza, ambaye kwa mujibu wa machapisho yao mtandaoni, ni wazi wanamngojea kwa hamu kubwa.

Wikiendi iliyopita wakati Dybala anasherehekea siku yake ya kuzaliwa akitimiza umri wa miaka 32, Oriana kupitia ukurasa wake wa Instagram alitoa ujumbe unaothibitisha hilo, alipoandika: "Heri ya siku ya kuzaliwa baby daddy wangu. Natumaini mwaka huu utakukuta ukiwa na utulivu, hamu ya mambo mapya, na mambo yote mazuri unayoyatafuta yakufikie moja kwa moja. 

"Huu ni mwaka wa mwisho tukiwa wawili tu. Nakupenda kwa moyo wangu wote!. Na Bebita (kijacho) pia, amenieleza hivyo kwa kunipiga teke moja (akiwa tumboni) wakati ninaandika haya."

Ikumbukwe Dybala alianza kucheza soka nchini Argentina akiwa na klabu ya Instituto kabla ya kuhamia Italia ambako alichezea Palermo, Juventus na kwa sasa akiitumikia Roma.

Ameshinda mataji mengi ya Serie A akiwa na Juventus na anahesabika kuwa miongoni mwa wafungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo aliyoichezea mechi zaidi ya 200 tangu 2015 hadi 2022.

Kwa mara ya kwanza aliitwa timu ya taifa ya Argentina mwaka 2015, na alikuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa Kombe la Dunia la Fifa 2022, ambapo alifunga moja ya mikwaju ya penalti katika fainali dhidi ya Ufaransa.

oriana 4

Ndoa yake na Oriana ilikuja baada ya mrembo huyo kufanya mambo mengi katika kiwanda cha sanaa akifuata nyayo za wazazi wake huku kazi zake zikimpatia mashabiki wengi hasa huko kwao. 

Oriana ni binti wa mfanyabiashara na mwigizaji wa zamani wa Argentina mwenye uraia wa Italia, Osvaldo Sabatini, na mama yake ni mwigizaji kutokea Venezuela, Catherine Fulop.

Akiwa amezaliwa Aprili 19, 1996 jijini Buenos Aires, Oriana ana mdogo wake aliyemzidi miaka mitatu aitwaye Tiziana Beatriz Sabatini. Pia ni mpwa wa bingwa maarufu wa tenisi duniani, Gabriela Sabatini.

Alianza mafunzo yake ya sanaa akiwa na umri mdogo, akijifunza kuimba, kupiga piano na uigizaji. Alisomea sanaa kwa miaka miwili katika taasisi ya Chavez, na mwaka mmoja, New York Film Academy.

Hata hivyo, tayari alikuwa ameshaanza kuzifukuzia ndoto zake kwani akiwa na umri wa miaka 13 alifanya kazi yake ya kwanza ya mitindo akitokea kwenye jarida lililochapisha makala kuhusu maisha yake na mama yake.

Mwaka 2017, alishiriki kwenye matangazo ya bidhaa za Casting Creme Gloss chini ya chapa ya L'Oreal. Hiyo ni baada kucheza tamthilia kwa mara ya kwanza, ambayo iliitwa Uruguay Porque te quiero asi hapo 2011.

Baadaye alicheza tamthilia nyingine, Aliados (2012), na kuanzia mwaka 2013 hadi 2014, alikuwa sehemu ya msimu wa vipindi vya vijana vya Aliados, miradi ambayo ilimjenga vilivyo kama mwigizaji.

Amecheza filamu kama Perdida (2018), filamu za Kihispania - Que te Juegas (2019), Rosario: Un clasico de amor y Futbol (2019) na kadhalika, huku akishiriki pia reality show kadhaa zilizorushwa kupitia televisheni.

oriana 3

Kwa upande wa muzuki, Oriana alijitosa katika tasnia hiyo kwa kuachia wimbo wake wa Kiingereza, Love Me Down Easy (2017), na miezi miwili baadaye akaitwa kuutumbuiza katika kipindi maarufu cha ShowMatch.

Ni wimbo uliopa nafasi ya kupanda jukwaani katika ziara ya mwanamuziki wa Marekani, Ariana Grande, Dangerous Woman Tour, ambapo aliimba pia nyimbo zake nyingine, Stay Or Run (2017) na What U Gonna Do (2018).

Mnamo 2018, alitumbuiza katika tamasha la Lollapalooza Argentina, akitumia jukwaa moja na bendi maarufu ya Marekani, Red Hot Chili Peppers, washindi wa tuzo za Grammy mara tatu.

Baada ya kuitii kiu yake katika mitindo, filamu na muziki, ndipo Oriana akafunga ndoa na Dybala, mchezaji mbunifu aliyepachikwa jina la La Joya (Lulu) kutokana na uwezo wake wa kudribble, mbinu, kasi na kufunga mabao.