Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Paula abadili gia angani kwa Marioo

Muktasari:

  • Paula, ambaye yupo kwenye uhusiano na staa wa Bongo Fleva Marioo, na tayari wamefanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike, awali aliwahi kuonyesha dalili za kuelekea kwenye ndoa, jambo lililowapa matumaini mashabiki wao.

PAULA Kajala, mtoto wa mwigizaji maarufu Kajala Masanja, ameibua mjadala mzito kwenye mitandao ya kijamii baada ya kubadilisha msimamo wake kuhusu ndoa, akisema kwa sasa hayupo tayari kuolewa kutokana na umri wake mdogo wa miaka 23.

Paula, ambaye yupo kwenye uhusiano na staa wa Bongo Fleva Marioo, na tayari wamefanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike, awali aliwahi kuonyesha dalili za kuelekea kwenye ndoa, jambo lililowapa matumaini mashabiki wao.

Katika kipindi cha nyuma, Paula aliwahi kuliambia Mwanaspoti na kuzungumza kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhusu mipango ya ndoa yao, huku wakionekana kuwa kwenye hatua nzuri ya kupeleka mahusiano yao mbele zaidi, hali iliyozua gumzo kubwa mitandaoni.

Hata hivyo, Mwanaspoti limezungumza na Paula kuhusu kauli zake mbili tofauti zilizowahi kuripotiwa. Alisema aliwahi kuweka wazi suala la ndoa, ila kwa sasa anaweka nguvu zaidi kwenye maisha yake binafsi na maendeleo yake.

“Masuala ya ndoa kwasasa nimebadili mawazo. Nimejitafakari na nimeona umri wangu bado haujafika wa kuwa kwenye ndoa. Mimi kwa sasa nimeelekeza nguvu zangu kwenye kutafuta fedha,” alisema Paula. Aidha, taarifa nyingine zilionyesha kuwa hata kwenye mipango ya ndoa, kulikuwa na mambo ya msingi kama dini na maandalizi binafsi ambayo yalihitaji muda kuyakamilisha. Paula alisema msimamo wake upo pale pale, na yuko tayari kubadili dini muda ukifika wa kuolewa.

Mabadiliko hayo ya msimamo yameibua hisia tofauti kwa mashabiki, ambapo baadhi wanamuunga mkono wakisema anafanya uamuzi sahihi wa kujipanga kwanza, huku wengine wakishangazwa na mabadiliko hayo, hasa baada ya dalili za awali za ndoa.