Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Big Phil na falsafa ya Pereira

Muktasari:

Alimtema Romario akiwa kwenye fomu yake ya mwisho mwaka 2002 kuelekea Korea ya Kusini na Japan, badala yake Ronaldo de Lima, Rivaldo, Gaucho, Luizao na Edilson wakiwa na damu changa, kasi kubwa na walikwishaliteka soka la dunia, pamoja na ukubwa wa jina na uwezo wa Romario alimpiga chini.

BIG Phil ametaja kikosi chake cha mwisho bila ya kumjumuisha Coutinho wa Liverpool, wapo wadau wa soka wengi wanalalamika kwa nini kijana asipewe nafasi kwenye kikosi, yawezekana wanaosema hivyo wakawa na hoja, lakini vipi kwa upande wa Luiz Felipe Scolari?

Alimtema Romario akiwa kwenye fomu yake ya mwisho mwaka 2002 kuelekea Korea ya Kusini na Japan, badala yake Ronaldo de Lima, Rivaldo, Gaucho, Luizao na Edilson wakiwa na damu changa, kasi kubwa na walikwishaliteka soka la dunia, pamoja na ukubwa wa jina na uwezo wa Romario alimpiga chini.

Hakumsikiliza hata Rais wa Brazil, Cordozo, leo anamtosa Coutinho, Sandro, Lucas Leiva, Lucas Moura na Kaka, swali la kujiuliza hapa ni moja tu, kwamba ukiwa na Willian, Oscar, Hulk, Bernad, hapa utamtoa nani ili aingie Coutinho?

Hili ndilo suala la kujiuliza, kwangu naona Big Phil yupo sahihi na nafikiri Coutinho atakuwa hazina ya baadaye ya Brazil, kwa sababu umri wake unamruhusu...angalia Kaka, Sandro na Lucas Leiva hawamo, Je, hawa kwa Luis Gustavo, Ramires, Fernandinho, Hernanes na Paulinho, nani atoke ili wao waingie? Labda kwangu ingizo lililonishangaza la Big Phil, ni huyu Henrique wa Napoli, kwingine sina shaka nako!

Big Phil amekuwa mtu muhimu sana kwa Wabrazil, kwani kipindi chake aliwaachia ubingwa wa dunia Wabrazil, pamoja na kelele nyingi za wapenzi wa kandanda wa nchi hiyo, kumkosoa kutokana na kikosi chake alichoteua kwa ajili ya fainali zilizofanyika nchi mbili kwa pamoja, Korea ya Kusini na Japan.

Amerejea tena na tayari kawapa Wabrazil ubingwa wa Kombe la Mabara, kwenye ardhi ya nyumbani, tena kwa kishindo, nani angekubali kwamba Hispania ilimaliza mechi ikiwa na mshangao?

Baada ya kuzabwa mabao 3-0 tena wakipigiwa kandanda la hali ya juu, ilikuwa fedheha kwa Mabingwa wa Dunia na Ulaya kwa kweli.

Ungesema nini kwa Wabrazil kwa shujaa huyu, ambaye sasa anatengeneza timu kwa kutumia jicho lake la tatu? Akitengeneza muunganiko mzuri kwa wachezaji wa nyumbani na wale wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya.

Angalia mifano ya vipaji vilivyopo kama Wilian, Fernandinho na Oscar ambao waliingia Ulaya wakiwa na nguvu ndogo, lakini sasa wametengeneza nguvu kwa kucheza ligi ngumu Ulaya.

Ni wazi kwamba Brazil imejaaliwa vipaji, lakini kikubwa kilichokosekana siku za karibuni ni nguvu kwa wanandinga wake na wengi wao kwa asilimia kubwa walilazimika kuzoea ligi kubwa za Ulaya baada ya muda mrefu, kabla ya kutengeneza kitu cha ziada kwenye ufundi wao.

Scolari anaweza kuwa kocha aliyefuata nyayo za Carlos Alberto Pereira ambaye kwa sasa ni mmoja wa wakurugenzi wa ufundi wa timu ya taifa aliyewahi kutengeneza mseto mkubwa wa wachezaji waliokuwa wanacheza Ulaya na wale wa nyumbani na zaidi ni kuwatumia wale waliokuwa wanacheza Ulaya kukabiliana na wanandinga wa Ulaya kwenye timu nyingine.

Hizo ndizo zilikuwa sababu za Pereira kuwa na nyota kama Carlos Dunga aliyekuwa nahodha wa kikosi kilichotwaa ubingwa kwa mara ya kwanza mnamo mwa 1994, tangia mwaka 1970.

Huyu alikuwa akicheza nchini Ujerumani na sasa ni falsafa ile ile inatumiwa na Scolari kujenga kikosi, naamini wenyeji wana nafasi..